DKT KIKWETE AKIRI SHERIA,HAKI NA UTAWALA BORA HUCHANGIA KUKUA KWA UCHUMI NA MAENDELEO KWA UJUMLA.

Na Janeth Raphael MichuziTv -Dodoma

RAIS Mstaafu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania wa awamu ya nne Mhe Dkt Jakaya Mrisho Kikwete amesema kuwa Maendeleo ya kiuchumi ya kijamii hustawi pale tu ambapo Utawala wa Sheria na Utawala bora vimetamaraki.

Dkt Kikwete ameyasema hayo Leo Jijini Dodoma katika Uzinduzi wa Wiki ya Sheria 20225 ulioratibiwa na Mahakama ya Tanzania.

Na kuongeza kuwa ni vigumu kwa jamii yenye Migogoro na kukosa Utawala wa Kisheria na Haki kuwa na mazingira rafiki ya kupata maendeleo endelevu.

“Ni ukweli usiopingika kwamba maendeleo ya kiuchumi ya kijamii hustawi pale tu ambapo Utawala wa Sheria na Utawala Bora vimetamaraki, ni vigumu kwenye jamii yenye Migogoro iliyokosa Utawala wa sheria, iliyokosa haki kuwa na mazingira rafiki ya kupata maendeleo endelevu kiuchumi na kijamii”.

Aidha Dkt Kikwete amempongeza Jaji Mkuu wa Mahakama na viongozi wote ndani ya mhimili huo kwa maboresho makubwa yanayoendelea kufanyika ikiwemo uboreshaji wa utoaji haki na kutokuwa ucheleweshwaji wa utoaji hukumu kama ilivyokuwa hapo awali.

“Napenda kutoa pongezi kwako Jaji Mkuu na viongozi wenzako wote kwa maboresho makubwa ambayo yanaendelea kufanyika ndani ya mhimili wa Mahakama hususani uboreshaji wa utoaji wa huduma za haki”.

Kwa upande wake Jaji Mkuu wa Tanzania Prof Ibrahim Juma ametumia wasaa huu kuzisihi Taasisi zote zilizopo katika mnyororo wa utoaji haki na zile zinazosimamia Haki madai kujipanga kutumia Dira mpya kufanya maboresho makubwa kama ambavyo Mahakama imejipanga kufanya maboresho makubwa kuliko waliyoyafanya sasa kuanzia hapo Januari mwaka ujao.

“Tunawasihi Taasisi zote zilizopo katika mnyororo wa utaji haki na Taasisi zote zinazosimamia haki madai zijipange kutumia Dira mpya kufanya maboresho makubwa, Sisi Mahakama tunajipanga vilevile kuhakikisha maboresho tunafanya maboresho makubwa kuliko ambayo tumefanya sasa kuanzia Januari mwaka ujao”.

Aidha amesema kuwa wiki hii ya Sheria hutumika kutoa Elimu kwa wananchi kwa lengo kuwawezesha kujua masula ya kisheria ili kujua kuzipambania stahiki zao, hivyo walitumie vizuri hili kwani watapata kujua mengi ikiwemo Katiba ya Nchi yao”.

“Siku ya Sheria Nchini hutanguliwa na wiki ya Sheria ambayo hutumika kutoa elimu ya Sheria kwa wananchi kwa lengo la kuwawezesha kujua masula mbalimbali ya kisheria ili kupambanua stahiki zao zilizo ndani ya Sheria na kutafuta namna ya kuzipata”.

“Wiki ya Sheria ni wiki mahsusi kwa elimu ya sheria kwa Umma, hivyo wananchi watumie kikamilifu wiki hii ya sheria kwasababu watapata kujua mambo mengi mbalimbali ikiwemo Katiba ya Nchi”.

Uzinduzi huu wa Wiki ya Sheria 2025 uliotanguliwa na Matembezi ya furaha yaliyokwenda kwa jina la Law Day Fun Run umeongozwa na kauli mbiu inayosema: “Tanzania ya 2025:Nafasi yavTaasisi zinazosimamia Haki Madai katika kufikia malengo Makuu ya Dira ya Taifa ya Maendeleo”.



Related Posts