Dodoma. Rais Mstaafu Jakaya Kikwete ameeleza namna changamoto ya ucheleweshaji wa kesi na utoaji wa nakala za hukumu ilivyokithiri na namna alivyopambana nalo wakati wa uongozi wake.
Amesema kuna kipindi kulikuwa na majaji waliokuwa na hukumu zaidi ya 60 ambazo hazijaandikwa, huku mmoja akiwa karibu kustaafu.
Simulizi hiyo ameitoa leo Jumamosi, Januari 25, 2025, alipohutubia baada ya matembezi na uzinduzi wa Wiki ya Sheria 2025 jijini Dodoma.
Amesema alipokuwa Rais, alitembelea taasisi mbalimbali ikiwamo Mahakama na kugundua malalamiko mengi kuhusu ucheleweshaji wa kesi na nakala za hukumu.
Mbali na Mahakama, amesema alitembelea Gereza la Keko jijini Dar es Salaam na kukutana na mfungwa aliyekaa miaka 10 akisubiri nakala ya hukumu, kitendo kilichomnyima fursa ya kukata rufaa.
“Lakini yote haya yalisababishwa na uhaba wa watumishi katika Mahakama, hivyo Serikali ilichukua hatua za kuongeza idadi ya majaji na mahakimu pamoja na kuwapatia mazingira bora ya kazi,” amesema Kikwete.
Amesema moja ya suluhisho lilikuwa kuanzisha Ofisi ya Mtendaji Mkuu wa Mahakama na Mfuko wa Mahakama ili kurahisisha upatikanaji wa rasilimali.
Hatua nyingine amesema ilikuwa kuwatenganisha wapelelezi na waendesha mashtaka ili kuboresha mchakato wa upelelezi.
Kuhusu majaji ambao walikuwa hawajaandika hukumu nyingi na mmoja wao akiwa karibu kustaafu, amesema Serikali iliamua kuwa jaji huyo asingestaafu hadi amalize kazi hiyo.
Hata hivyo, amesema changamoto kama hizo sasa zimetatuliwa kwa kiasi kikubwa, hasa kupitia matumizi ya teknolojia, ikiwamo akili bandia.
Akizungumza kwenye hafla hiyo, Jaji Mkuu wa Tanzania, Profesa Ibrahim Juma amesisitiza umuhimu wa Mahakama na taasisi zake zote zinazohusika katika utoaji haki kujipanga kwa maboresho makubwa zaidi yatakayosaidia utekelezaji wa Dira ya 2050 ambayo utekelezaji wake utaanza mwaka ujao.
“Sisi Mahakama tunajipanga kuhakikisha maboresho yanayotekelezwa baada ya Dira ya 2025 yatakuwa makubwa zaidi,” amesema Profesa Juma.
Mkurugenzi Msaidizi wa Ofisi ya Mwendesha Mashtaka Mkuu wa Serikali (OTM), Renatus Mkude amesema changamoto ya ucheleweshaji wa kesi imepungua kwa kiasi kikubwa kupitia miongozo na sheria zilizoweka ukomo wa muda.
“Sasa hivi, mashauri hayaendi mahakamani bila upelelezi kukamilika. Tumepokea mwongozo wa kukamilisha upelelezi ndani ya siku 90, na ziara za Mkurugenzi wa Mashtaka magerezani zimepunguza malalamiko,” alisema Mkude.
Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Usimamizi wa Kesi na Udhibiti Ubora, Camilius Ruhinda, alisema kuwa Ofisi ya Wakili Mkuu wa Serikali imeanzisha mifumo ya usimamizi wa kesi kwa kutumia teknolojia. “Kesi zote za Serikali zinapangwa na kusimamiwa kupitia mfumo huu, ambao upo ofisi zote nchini,” amesema.
Mbali na hayo, Mamlaka ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya (DCEA) ilibainisha kuwa kuna dawa mpya za kulevya 1,258 ambazo bado haziko chini ya udhibiti wa kisheria.
Kamishna wa Ukaguzi na Sayansi ya Jinai wa Mamlaka ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya (DCEA), Dominic Dormician amesema uhalifu unaongezeka kadri teknolojia inavyokua, ikiwemo kuibuka kwa aina mpya ya dawa za kulevya.
“Kuna dawa mpya 1,258 ambazo hazidhibitiwi kisheria. Kazi yetu ni kufanya utafiti na kutoa mapendekezo ya dawa hizi mpya kuingizwa kwenye jedwali la sheria ili kudhibiti matumizi yake,” amesema.
Amesema kuna kemikali 33 zinazodhibitiwa kisheria, lakini nje ya sheria kuna zaidi ya kemikali 90 zinazotumika kutengeneza dawa za kulevya.
Dormician pia amebainisha kuwa hata dawa tiba zimekuwa changamoto, kwa sababu wahalifu hutumia mianya iliyopo kukwepa mkondo wa sheria.
Hakimu Mkazi Mkuu, Denice Mlashani, Msimamizi wa Kituo cha Huduma kwa Wateja cha Mahakama ya Tanzania, amesema mwaka uliopita wamepokea maoni 1,806 kutoka kwa wananchi na asilimia kubwa ya malalamiko yalihusiana na masuala ya mirathi.
“Wajane na watoto wa nje ya ndoa mara nyingi hawapewi haki zao. Wasimamizi wa mirathi wamekuwa wakitumia nafasi hiyo kujinufaisha kwa mali zinazopaswa kugawanywa kwa haki,” amesema Mlashani.
Ameongeza kuwa Mahakama imejipanga kushirikiana na wadau mbalimbali ili kuangalia namna bora ya kushughulikia migogoro ya mirathi na kupunguza changamoto hizi kwa wananchi.
Dodoma. Rais Mstaafu Jakaya Kikwete ameeleza namna alivyoshughulikia ucheleweshaji wa kesi na utoaji wa nakala za hukumu wakati wa uongozi wake.
Amesema kuwa kulikuwa na majaji waliokuwa na hukumu zaidi ya 60 ambazo bado hazijaandikwa, huku mmoja akiwa karibu kustaafu.
Kauli hiyo ameitoa leo Jumamosi, Januari 25, 2025, alipohutubia baada ya matembezi na uzinduzi wa Wiki ya Sheria, 2025 jijini Dodoma. Amesema alipokuwa Rais, alitembelea taasisi mbalimbali ikiwamo mahakama na kugundua malalamiko mengi kuhusu ucheleweshaji wa kesi na nakala za hukumu.
Kikwete amesema alitembelea Gereza la Keko, Dar es Salaam na kukutana na mfungwa aliyekaa miaka 10 akisubiri nakala ya hukumu, hali iliyomnyima fursa ya kukata rufaa.
“Lakini yote haya yalisababishwa na uhaba wa watumishi katika mahakama, hivyo serikali ilichukua hatua za kuongeza idadi ya majaji na mahakimu, pamoja na kuwapatia mazingira bora ya kazi,” amesema Kikwete.
Amesema moja ya suluhisho lilikuwa kuanzisha Ofisi ya Mtendaji Mkuu wa Mahakama na Mfuko wa Mahakama ili kurahisisha upatikanaji wa rasilimali.
Hatua nyingine amesema ilikuwa kuwatenganisha wapelelezi na waendesha mashtaka ili kuboresha mchakato wa upelelezi.
Rais Kikwete ametaja pia kwamba, kulikuwa na majaji ambao hawajaandika hukumu nyingi na mmoja wao akiwa karibu kustaafu.
Serikali iliamua kuwa jaji huyo asingestaafu hadi amalize kazi hiyo. Amesema changamoto kama hizo sasa zimetatuliwa kwa kiasi kikubwa, hasa kupitia matumizi ya teknolojia, ikiwamo akili bandia, katika mchakato wa mahakama.
Mbali na hayo Mamlaka ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya (DCEA) ilibainisha kuwa kuna dawa mpya za kulevya 1,258 ambazo bado haziko chini ya udhibiti wa kisheria.
Suala la ucheleweshaji kesi limegusiwa pia na Mkurugenzi Msaidizi wa Ofisi ya Mwendesha Mashtaka Mkuu wa Serikali (OTM), Renatus Mkude aliyesema changamoto hiyo imepungua kwa kiasi kikubwa kupitia miongozo na sheria zilizoweka ukomo wa muda.
“Sasa hivi, mashauri hayaendi mahakamani bila upelelezi kukamilika. Tumepokea mwongozo wa kukamilisha upelelezi ndani ya siku 90 na ziara za Mkurugenzi wa Mashtaka magerezani zimepunguza malalamiko,” alisema Mkude.
Kuhusu matumizi ya teknolojia, Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Usimamizi wa Kesi na Udhibiti Ubora, Camilius Ruhinda, amesema Ofisi ya Wakili Mkuu wa Serikali imeanzisha mifumo ya usimamizi wa kesi kwa kutumia teknolojia.
“Kesi zote za Serikali zinapangwa na kusimamiwa kupitia mfumo huu, ambao upo ofisi zote nchini,” amesema.
Akizungumza kwenye hafla hiyo, Bottom of Form
Jaji Mkuu wa Tanzania, Profesa Ibrahim Juma amesisitiza umuhimu wa Mahakama na taasisi zake zote zinazohusika katika utoaji haki kujipanga kwa maboresho makubwa zaidi yatakayosaidia utekelezaji wa Dira ya 2050, ambayo utekelezaji wake utaanza mwaka ujao.
“Sisi Mahakama tunajipanga kuhakikisha maboresho yanayotekelezwa baada ya Dira ya 2025 yatakuwa makubwa zaidi,” amesema Profesa Juma.
Hakimu Mkazi Mkuu, Denice Mlashani Msimamizi wa Kituo cha Huduma kwa Wateja cha Mahakama ya Tanzania, amesema mwaka uliopita walipokea maoni 1,806 kutoka kwa wananchi na asilimia kubwa ya malalamiko yalihusiana na masuala ya mirathi.
“Wajane na watoto wa nje ya ndoa mara nyingi hawapewi haki zao. Wasimamizi wa mirathi wamekuwa wakitumia nafasi hiyo kujinufaisha kwa mali zinazopaswa kugawanywa kwa haki,” amesema Mlashani.
Kutokana na hilio, amesema Mahakama imejipanga kushirikiana na wadau mbalimbali ili kuangalia namna bora ya kushughulikia migogoro ya mirathi na kupunguza changamoto hizi kwa wananchi.
Katika hatua nyingine, Kamishna wa Ukaguzi na Sayansi ya Jinai wa Mamlaka ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya (DCEA), Dominic Dormician ameiarifu hafla hiyo kuwa uhalifu unaongezeka kadri teknolojia inavyokua, akibainisha kuibuka kwa aina mpya ya dawa za kulevya.
“Kuna dawa mpya 1,258 ambazo hazidhibitiwi kisheria. Kazi yetu ni kufanya utafiti na kutoa mapendekezo ya dawa hizi mpya kuingizwa kwenye jedwali la sheria, ili kudhibiti matumizi yake,” amesema.
Amesema kuna kemikali 33 zinazodhibitiwa kisheria, lakini nje ya sheria kuna zaidi ya kemikali 90 zinazotumika kutengeneza dawa za kulevya.
Dormician pia amebainisha kuwa hata dawa tiba zimekuwa changamoto, kwa sababu wahalifu hutumia mianya iliyopo kukwepa mkondo wa sheria kwenye matumizi yake.