Mganga mbaroni kwa tuhuma ya kumiliki fisi, aeleza anavyomtumia

Bariadi. Jeshi la Polisi Mkoa wa Simiyu limemkamata Emanuel Maduhu (31) mkazi wa Kijiji cha Kilulu, Kata ya Bunamala, Wilaya ya Bariadi ambaye ni mganga wa kienyeji kwa tuhuma ya kumiliki fisi aliye hai.

Taarifa iliyotolewa na Kamanda wa Polisi Mkoa wa Simiyu, Edith Swebe  leo Jumamosi Januari 25, 2025 imeeleza kuwa mganga huyo alidai kumtumia fisi huyo kama chombo cha usafiri

“Mganga huyo alieleza kuwa anamtumia fisi huyo katika shughuli za uganga wa jadi ikiwa ni pamoja na kumtumia kama chombo cha usafiri anapotaka kupaa angani.

“Jeshi la Polisi kwa kushirikiana na mamlaka za wanyamapori wanaendelea na uchunguzi na mara baada ya upelelezi kukamilika mtuhumiwa atafikishwa mahakamani,” imeeleza taarifa hiyo.

Kamanda Edith ametoa wito kwa wananchi kuacha mara moja kufuga fisi, kwani wanyama hao ni hatari na siku za hivi karibuni kumekuwa na wimbi kubwa la watoto kuliwa na fisi.

Related Posts