WATALII MILIONI 1. 8 WAMETEMBELEA HIFADHI ZA TAIFA NCHINI MWAKA 2023/24

Na Janeth Raphael MichuziTv – Morogoro

Sekta ya utalii nchini imeelezwa kuchangia ongezeko kubwa la idadi ya watalii, sambamba na ongezeko la uwekezaji na mapato yatokanayo na utalii, ambapo kumekuwa na ongezeko la safari za ndege za moja kwa moja kutoka maeneo mbalimbali ya dunia kuja Tanzania kupitia mashirika makubwa ya ndege Duniani.

Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo na Msemaji Mkuu wa Serikali ,.Gerson Msigwa ameyazungumza hayo leo na waandishi wa habari wa Mkoa wa Dodoma na Morogoro akielezea utekelezaji wa Serikali wakati wa Mkutano uliofanyika leo Januari 25,2025 katika Hifadhi ya Taifa ya Mikumi,Morogoro.

Amesema utalii kwenye Hifadhi za Taifa umeendelea kukua pia idadi ya watalii na mapato yameongezeka mwaka hadi mwakaa, Msigwa amesema Takwimu zinaonesha kuwa mwaka 2023/2024 watalii milioni 1,863,108 walitembelea hifadhi za Taifa.

Hata hivyo amesema kuwa watalii wameengezeka,Idadi hii imeongezeka ikilinganishwa na watalii milioni 1,618,538 waliotembelea Hifadhi za Taifa mwaka 2022/2023 ambalo ni ongezeko la watalii 244,570 sawa na asilimia 15.1.

Vilevile, kwa Mwaka wa Fedha 2024/2025 Shirika lilikadiria kupokea watalii milioni 1,848,759 ambapo kwa kipindi cha miezi sita Julai – Disemba 2024 watalii milioni 1,146,438 walitembelea Hifadhi za Taifa ambayo ni sawa na asilimia 62 ya makadirio ya mwaka.

Amesema ongezeko hilo la watalii limeenda sambamba na ongezeko la mapato ambapo kwa kipindi cha Julai – Juni 2023/2024, Serikali kupitia TANAPA lilipanga kukusanya shilingi bilioni 382,307,977,497.07 na limefanikiwa kukusanya Shilingi bilioni 410,903,648,082.3 ambayo ni sawa na ongezeko la asilimia 7.5 ya mapato yaliyokusudiwa kukusanywa kwa kipindi husika.

“Mapato hayo ni ongezeko la asilimia 21.8 ukilinganisha na 2022/2023 ambapo kiasi cha Shilingi 337,424,076,896.29 zilikusanywa,”amesema Msigwa

Aidha, katika mwaka wa fedha 2024/2025 Serikali kupitia TANAPA lilikadiria kukusanya kiasi cha Shilingi bilioni 430,864,198,480, ambapo katika kipindi cha miezi sita Julai hadi Disemba 2024 Shirika limekusanya kiasi cha Shilingi bilioni 325,146,978,076.63 sawa na asilimia 75.5 ya malengo ya makusanyo ya mwaka.





Related Posts