Mlandizi Quens ni maombi tu ikijipanga upya

HALI iliyonayo mabingwa wa zamani wa Ligi ya Wanawake (WPL), Mlandizi Queens siyo nzuri na sasa inasuka mipango mipya kuhakikisha mechi nane zilizosalia ni kufa na kupona.

Hadi sasa Mlandizi haijaonja ladha ya ushindi tangu ishiriki ligi ikisalia mkiani mwa msimamo na pointi moja ikiruhusu mabao 50 na kufunga tano.

Akizungumza na Mwanaspoti, Kocha wa timu hiyo, Jamila Hassan alisema ili kusalia ligi hiyo anapaswa kuandaa mikakati madhubuti kwani iko kwenye hali mbaya.

Aliongeza kwanza lazima awaandae wachezaji kiakili pamoja na mipango ya kushinda mechi zilizosalia ambazo siyo rahisi kwao.

“Tangu mwanzo nilisema kipindi kile na sasa ni tofauti, ligi imekuwa na ushindani sana, matamanio yetu kuendelea kusalia ligi kuu ili msimu ujao tujiandae vyema lakini ni ngumu sana,” alisema Jamila na kuongeza

“Sababu kubwa ya sisi kutofanya vizuri ni pamoja na changamoto ya vibali, umeona hata mechi ya juzi wachezaji wa akiba walikuwa watano tofauti na wenzetu.”

Ikumbukwe hawa ni mabingwa wa kihistoria wa ligi hiyo ikichukua ubingwa msimu 2017/18 na tangu hapo JKT Queens na Simba Queens zimekuwa ikitawala.

Related Posts