Vibali Gets Program vyasimamisha Mchezo

MCHEZO wa raundi ya 10 Ligi ya Wanawake juzi kati ya Get Program na Mashujaa Queens ulishindwa kuendelea huku sababu ikiwa ni pamoja na changamoto ya vibali.

Mchezo huo ulipigwa Uwanja wa Jamhuri Dodoma uliishia dakika 39 huku Mashujaa akiongoza kwa mabao 4-0.

Get Program inakabiliwa na changamoto kwa baadhi ya vibali na kusababisha kuchezesha wachezaji tisa dhidi ya 11 kwa wapinzani wao.

Hata hivyo, idadi ya wachezaji hao ilipungua baada ya mchezaji mmoja wa Get kuumia na kuwafanya wabaki nane jambo lilomfanya mwamuzi wa mchezo kuuahirisha.

Mwanaspoti tulipomtafuta Ofisa Habari wa Shirikisho la Soka nchini (TFF), Clifford Ndimbo alisema kanuni na sheria zitafuatwa juu ya changamoto hiyo.

“Tunafahamu lakini ligi inaendeshwa na sheria zake, kanuni tu inaelekeza maana ni jambo la kikanuni,” alisema Ndimbo.

Hata hivyo, Mwanaspoti lilimtafuta mratibu wa Get Program lakini hakupokea simu.

Kanuni ya soka la wanawake Sura ya tano kanuni ya 18 kifungu cha 25 kinaeleza ikithibitika ushindi inapewa timu pinzani.

“Iwapo itathibitika bila kujali kukatwa au kutokatwa rufaa, kupitia taarifa za mchezo za kamishna ama kwa njia yoyote kuwa timu imechezesha mchezaji ambaye

hajaorodheshwa kwenye fomu maalum ya orodha ya wachezaji na viongozi kama mchezaji wa siku hiyo kwa mchezo husika na hivyo kushindwa kupitia mchakato wa ukaguzi wa wachezaji kabla ya mchezo, timu hiyo itapoteza mchezo na ushindi kupewa timu pinzani.”

Related Posts