WAZIRI JAFO ATAKA HUDUMA KWA WAKATI ZAHANATI YA BWAMA.

Waziri wa Viwanda na Biashara na Mbunge wa Jimbo la Kisarawe Mhe. Dkt.Selemani Jafo(Mb) amemtaka Mganga Mkuu wa Wilaya ya Kisarawe kuhakikisha huduma ya Afya inapatikana wakati wote katika Zahanati ya Bwama.

Amebainisha hayo wakati anazindua Zahanati ya Bwama iliyopo Wilaya ya Kisarawe Janauri 25,2025 ambapo amesisitiza huduma hiyo ya utaoji wa afya isisimame ili wananchi waweze kupata huduma hiyo waliokuwa wanaipata kutoka mbali na kijiji hicho.

Aidha Dkt.Jafo amemuagiza Mkurugenzi wa Halmashauri ya Kisarawe kuziagiza taasisi za RUWASA kuhakikisha wanachimba kisima katika Zahanati hiyo ili kiweze kusaidia upatikanaji wa maji katika zahanati na matumizi kwa wananchi pamoja kuiagiza TARURA kuhakikisha barabara inayounganisha kijiji hicho inafanyiwa ukarabati kwa haraka pamoja na kuagiza taasisi zote zishiriki katika ziara zake.

Vilevile Dkt.Jafo amesema Serikali kupitia ilani ya Chama cha Mapinduzi (CCM) inaendelea kuwajali wananchi wa Kisarawe kwa kuhakikisha huduma zote muhimu zinapatikana kwa kujenga miundombinu ya huduma hizo kwenye kila kila Kata na Vijiji kama vile afya,nishati na elimu katika jimbo hilo la Kisarawe kwani karibia Kata zote zimefikiwa.

Pia Dkt.Jafo amewaasa Wananchi wa Kisarawe kuhakikisha wanawapeleka watoto wao wa Sekondari hosteli ili wakae maeneo ya karibu na shule ili kupata elimu kwa ukaribu kwani Serikali imefanya maendeleo makubwa ya ujenzi wa shule za Sekondari nane pamoja hosteli kwa muda mfupi.

Related Posts