WIZARA ya Afya nchini imesema kuwa imechukua tahadhali zote zinazohusu masuala ya afya kwa ajili ya kuwahudumia viongozi na wageni mbalimbali watakaohudhuria Mkutano Mkuu wa Nishati Barani Afrika utakaoanza kesho tarehe 27 Januari 2025.
Akizungumza leo 26 Januari 2025, kwenye Hospitali ya Agha Khan ikiwa ni ziara ya ukaguzi wa hospitali mbalimbali zilizoandaliwa kwa ajili ya kuhudumia wageni hao, Waziri wa Afya,Jenister Mhagama amesema nchi imejianda vizuri katika eneo hilo kwa ajili ya kuwahudumia wageni watakaopata dharula kiafya.
“Kama tunavyofahamu tutakuwa na mkutano mkubwa uaaohusiana na masuala ya nishati lakini tumeshuhudia nchi yetu ikipokea wageni wengi na hasa viongozi wakubwaa kutoka katika nchi mbalimbali barani Afrika pamoja na Taasisi zinazojihusisha na masuala ya Nishati”, amesema Mhagama.
Ameongeza,”Tumejiandaa na kuchukua tahadhari ya kutoa matibabu ya aina yoyote kwa jambo lolote ambalo litatokea kipindi hiki mkutano utakapokuwa ukiendelea hivyo leo nikiwa nimeambatana na Katibu Mkuu na baadhi ya viongozi kutoka kwenye taasisi za tiba nchini imetupasa kuja kukagua taasisi moja badaa ya nyingine na kujihakikishia kama maandalizi yetu yapo tayari kuwapokea wageni tumeanza hapa Agha Khan kwa kweli niwahakikishie wapo tayari tena katika viwango vya hali ya juu,”
Mhagama amesema kuwa Hospitali ya Agha Khan imekamilika kwenye huduma za matibabu kila idira “Tumekagua emergency kwa kweli eneo la dharula liko vizuri , ICU maeneo ya vifaa tiba yako vizuri kila kitu kipo vizuri “.
Waziri amesema kuwa Serikali ya Tanzania itautumia mkutano huo kutangaza utalii wa tiba.
Mganga Mkuu wa Taasisi ya Afya ya Agha Khan Dkt Harrison Chuwa amesema kuwa Hospitali yao imejiandaa kwa ajili ya kutoa huduma kwa viongozi waliohudhuria mkutano wa Nishati safi Afrika.
“Tumejiandaa kwa ajili kuwahudumia wageni wetu sisi tumepokea kwa mikono miwili jukumu la kuwa moja ya hospitali itakayowahudimia viongozi waadhamizi waliohudhuria Mkutano mkuu wa Nishati”, amesema Chuwa
Dkt Chuwa amesema kuwa serikali imejiridhisha kuwa hospitali hiyo inastahili kuwahudumia wageni hao wenye hadhi.
Waziri wa Afya Jenista Mhagama (katikati) akizungumza na Waandishi wa Habari mara baada ya kumaliza ukaguzi katika Hospitali ya Agha Kan na kujionea jinsi Hospitali hiyo ilivyojiandaa ili kukabiliana na changamoto yoyote itakayojitokeza kwa wageni watakaohudhuria Mkutano wa Nishati Barani Africa. Mkutano huo wa siku mbili utaanza kesho Januari 27, 2025 na kumalizika Januari 28,2025 jijini Dar es Salaam
Mganga Mkuu wa Hospitali ya Agha Kan, Dkt. Harison Chuwa akizungumza na Waandishi wa Habari mara baada ya Wiziri wa Afya Jenista Mhagama kumaliza ukaguzi katika Hospitali hiyo na kujionea jinsi walivyojiandaa ili kukabiliana na changamoto yoyote itakayojitokeza kwa wageni watakaohudhuria Mkutano wa Nishati Barani Africa. Mkutano huo wa siku mbili utaanza kesho Januari 27, 2025 na kumalizika Januari 28,2025 jijini Dar es Salaam