WAZIRI WA ULINZI NA JKT AFANYA ZIARA WILAYANI MONDULI KUONGEA NA VIONGOZI WA JAMII YA WAFUGAJI

Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa Mhe Dkt Stergomena Tax (Mb) amefanya ziara ya Kikazi katika Wilaya ya Monduli mkoani Arusha, na kufanya mazungumzo na Viongozi wa Kimila wa jamii ya Kimasai, Viongozi wa Vijiji na Madiwani, katika Ukumbi wa Halmashauri ya wilaya ya Monduli.
Mkutano huo wa Waziri wa Ulinzi na JKT ulikuwa na lengo la kujadili matumizi bora ya ardhi kati ya jamii ya Wafugaji wa Wilaya ya Monduli pamoja na kujadili changamoto mbalimbali za matumizi ya ardhi wilayani Monduli, ambazo zimejitokeza katika siku za karibuni, aidha Mhe Waziri Tax alipata fursa ya kupata taarifa zinazohusu Mafunzo ya Kijeshi katika eneo hilo.
Akimkaribisha Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa, kuongea na halmashauri ya wilaya ya Monduli na viongozi wa jamii ya wafugaji, Mbunge wa Jimbo la Monduli, Mhe Fred Lowassa,amemshukuru Waziri wa Ulinzi na JKT kwa kufika wilayani Monduli kwa haraka baada ya kuombwa kufanya hivyo naye, kuja kujadiliana na viongozi wa kimila wa jamii ya wafugaji na wakulima wa wilaya ya Monduli, na namna bora ya kutatua changamoto zinazohusiana na matumizi ya ardhi na kuimarisha uhusiano wa muda mrefu baina ya Jeshi la Wananchi wa Tanzania pamoja na wananchi.
Akiongea katika kikao hicho cha viongozi wa kimila wa jamii ya wafugaji pamoja na uongozi wa halmashauri ya Monduli, Waziri Tax amewahakikishia wananchi wa wilaya ya Monduli kwamba matumizi salama ya ardhi yataendelea kuwepo kama ilivyokuwa awali katika maeneo yanayomilikiwa na JWTZ na akawataka wananchi wa eneo hilo kuhakikisha mahusiano mahusiano mazuri yaliyopo kati yao na Jeshi la Wananchi yanaendelea kudumu na kuimarishwa. Aidha Waziri Tax amewaambia wananchi wa eneo la Monduli kuwa taratibu zote za kisheria ili kila mtu apate haki yake na kwa usawa zitafuatwa.
Mkutano huo wa Waziri wa Ulinzi na JKT ulihudhuriwa pia Mkuu wa Wilaya ya Monduli, Mhe Festo Shem Kiswaga pamoja na viongozi wa jamii ya wafugaji wa jamii ya Kimasai, halmashauri ya mjii wa Monduli,na viongozi waandamizi toka Jeshi laUlinzi la Wananchi wa Tanzania.

Related Posts