Waziri wa Fedha,
Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba (Mb) (Kushoto), akisalimiana na Rais
wa Benki ya Dunia, Bw. Ajay Banga, kando ya Mkutano wa Nishati wa Wakuu
wa nchi na Serikali wa Afrika, ulioanza tarehe 27 Januari 2025 katika
Kituo cha Kimataifa cha Mikutano Cha Julius Nyerere (JNICC), Jijini Dar
es Salaam. Mkutano huo unaotarajiwa kutamatika tarehe 28 Januari 2025
utawakutanisha Wakuu wa Nchi za Afrika na wadau muhimu wa sekta ya
nishati ili kujadili mikakati ya kuhakikisha upatikanaji wa nishati ya
uhakika, nafuu, na endelevu kwa maendeleo ya Bara la Afrika.
(Picha na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini, WF, Dar es Salaam)