HAJI M.MNASI,PhD AZINDUA KITABU CHA MALEZI YA WATOTO ZAMA ZA KIDIGITALI

Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Siha, Dk Haji Mnasi amezindua  kitabu cha Elimu na malezi  Kwa Watoto katika Zama Za Kidijitali ambapo jamii kubwa imekumbwa na changamoto ya malezi na makuzi kwa watoto.

Dk Mnasi  amezindua kitabu hicho cha Elimu na Malezi Kwa Watoto katika Zama Za kidigitali katika kijiji cha Kitangari Sokoni kilichopo wilayani Newala mkoani Mtwara, Uzinduzi wa kitabu hicho umefanya Jana Tar 25/01/2025 katika Viwanja vya Mpira shule ya msingi Kitangari B. 

Dkt Mnasi amemshukuru Mh Rais wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania Dkt Samia Suluhu Hassan Kwa kuendelea kumuamini huku akisema licha ya Kuwa na majukumu mengi ya kiserikali ila aliwiwa kuandika kitabu hicho cha Elimu na Malezi Kwa Watoto katika Zama Za kidigitali kutokana na Kasi kubwa ya ukuwaji wa utandawazi ambao Kwa kiwango kikubwa unaathiri Mila na tamaduni Kwa Jamii yetu .

Amesema hivyo kitabu hicho kinaenda Kuwa suluhisho katikati zama hizi za utandawazi na ukuwaji wa technologijia hivyo amewataka wazazi, walezi pamoja na Jamii kupata Nakala za kitabu hicho ili kuwasaidia watoto katika namna Bora ya kujifunza na kupata Elimu pamoja na Malezi yaliyo bora ili kukuza Taifa lenye maadili mema, uchapakazi kama ambavyo maono ya Mh Rais Samia Suluhu yamekua yakijikita katika kusisitiza ujenzi wa Jamii bora na kizazi salama cha kesho.

Related Posts