Dar es Salaam. Leo Januari 27, umeanza mkutano wa kimataifa wa siku mbili kuhusu nishati Afrika unaowakutanisha viongozi mbalimbali wa bara hili, unaendelea hivi sasa katika Kituo cha Mikutano cha Julius Nyerere (JNICC), jijini Dar es Salaam.
Mkutano huo unashirikisha viongozi wengi wa Bara la Afrika unajadili mambo mbalimbali kuhusu nishati huku ukiwa na mjadala mbalimbali pamoja na watoa mada.
Kupeleka ajenda ya nishati Afrika kwa kiwango cha juu
Mada: Je, Misheni 300 inachukua hatua gani kuinua upatikanaji wa nishati barani Afrika? Kwa nini kampuni zinapaswa kuwekeza? Kwa nini serikali zinapaswa kufanya mabadiliko ya sera? Na kwa nini washirika zaidi wanapaswa kushiriki? Mafanikio ya mkutano huu yangekuwaje?
• Rais wa Benki ya Maendeleo ya Afrika, Dk Akinwumi Adesina
• Rais wa Benki ya Dunia, Ajay Banga
• Rais wa Taasisi ya Rockefeller, Dk Rajiv Shah
Mwendeshaji: Mtangazaji wa kituo cha televisheni cha CNN International ya Marekani, Zain Asher
Mada: Sera na mageuzi kwa kubadilisha sekta ya nishati Afrika
Je, watunga sera wanapanga vipi kufanikisha upatikanaji wa nishati kwa wote, iliyo ya kuaminika na endelevu ifikapo mwaka 2030? Je, mifumo ya sera na taasisi inaweza kuimarishwa vipi kuvutia ushiriki mkubwa wa sekta binafsi katika uwekezaji wa nishati? Serikali inapaswa kuchukua jukumu gani katika mageuzi ya huduma za umeme ili kuboresha uendelevu wa sekta?
Makamu wa Rais wa Nguvu, Nishati, Hali ya Hewa, na Ukuaji wa Kijani wa Benki ya Maendeleo ya Afrika, Dk Kevin Kariuki.
- Waziri wa Madini, Petroli na Nishati, Jamhuri ya Côte d’Ivoire, Mamadou Sangafowa-Coulibaly.
- Waziri wa Fedha na Waziri wa Uratibu wa Uchumi wa Nigeria, Wale Edun.
- Waziri wa Nishati na Petroli wa Kenya, Opiyo Wandayi.
- Waziri wa Fedha na Mipango ya Kitaifa wa Zambia, Dk Situmbeko Musokotwane.
- Waziri wa Mpito wa Nishati na Maendeleo Endelevu wa Morocco, Dk Leila Benali.
- Waziri wa Fedha, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC), Doudou Fwamba Likunde Li-Botayi.
Mwendeshaji: Mkurugenzi Mtendaji na Mwakilishi Maalumu wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa kwa Nishati Endelevu kwa Wote, Damilola Ogunbiyi.
Endelea kufuatilia Mwananchi.