Wapelistina Wahamishwe Gaza – Global Publishers


Rais Donald Trump wa Marekani

Rais Donald Trump wa Marekani amependekeza Wapalestina wa Ukanda wa Gaza wahamishwe katika ardhi yao hiyo na kupelekwa nchi jirani kama Misri na Jordan.
Pendekezo lisilo la kawaida ambalo lilipingwa hata na utawala wa mtangulizi wake Joe Biden.

Akizungumza na waandishi wa habari ndani ya ndege ya Air Force One wakati anaelekea Miami, Trump amesema, alizungumzia suala hilo wakati wa mazungumzo ya simu aliyofanya na Mfalme Abdullah II wa Jordan, na huenda akalizungumzia tena atakapowasiliana na Rais wa Misri Abdel-Fattah al-Sisi.

“Nilimwambia (mfalme wa Jordan) kwamba ningependa uwachukue wengine wengi zaidi kwa sababu nikiangalia Ukanda wote wa Gaza hivi sasa ni fujo, ni fujo hasa,” amedai rais huyo wa Marekani na kuongezea kwa kusema: “Ningependa yeye (mfalme wa Jordan) achukue watu”.

Katika mahojiano hayo aliyofanyiwa jana Januari 26, Trump ameendelea kueleza: “Ningependa Misri ichukue watu, Nitazungumza na Jenerali Al Sisi kesho Ningependa Misri ichukue watu. Na ningependa Jordan ichukue watu”.

“Unazungumza kuhusu watu milioni moja na nusu, tusafishe tu sehemu yote hiyo. Unajua kwa karne nyingi kumekuwa na migogoro mingi. Lazima kitu kifanyike”, amesisitiza Trump kwa kauli inayoashiria kuwa lengo lake ni kuwahamisha Wapalestina huko Gaza, suala ambalo ndilo linalotiliwa mkazo pia na utawala wa Israel.

Huku akiitaja Ghaza kama “eneo la kubomolewa,” Rais huyo wa Marekani amesema, anapendelea kushirikiana na baadhi ya mataifa ya Kiarabu na kujenga nyumba katika eneo jengine tofauti ili Wapalestina waweze kuishi huko; na akaongeza kuwa hatua hiyo inaweza kuwa ya muda mfupi au inaweza kuwa ya muda mrefu.

Itakumbukwa kuwa serikali ya Biden ilipinga kuwahamisha wakazi wa Ghaza nje ya eneo hilo, na kutetea kurejeshwa Wapalestina kwenye makazi yao sambamba na kuwepo uwezekano wa kufika.

Related Posts