Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Niger, Mheshimiwa Ali Mahaman Lamine Zeine, amewasili jijini Dar es Salaam kwa ajili ya kushiriki Mkutano wa Kilele wa Wakuu wa Nchi za Afrika kuhusu Nishati, unaotarajiwa kufanyika tarehe 27 hadi 28 Januari 2025.
Katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere, Mheshimiwa Zeine amepokelewa na Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Cosato Chumi.
Mkutano wa Kilele wa Wakuu wa Nchi unalenga kuimarisha juhudi za pamoja katika kukabiliana na changamoto za nishati barani Afrika, sambamba na kupitisha Azimio la Dar es Salaam, linalosisitiza dhamira ya Viongozi wa Nchi na Serikali za Afrika kuhakikisha upatikanaji wa nishati ya uhakika, nafuu, na endelevu barani Afrika.