Maafisa Waliomfungulia Kesi Trump, Wafutwa Kazi – Global Publishers



Rais wa Marekani Donald Trump

Maafisa wa Wizara ya Sheria nchini Marekani wamewafuta kazi waendesha mashtaka kadhaa waliozishughulikia kesi za jinai zilizomkabili Rais Donald Trump. Maafisa hao wamesema hawawezi kuwaamini waendesha mashtaka hao.

Wafanyakazi hao walihusika katika uchunguzi wa Mwanasheria Maalum Jack Smith uliosababisha kufunguliwa mashtaka ambayo sasa yametupiliwa mbali dhidi ya Trump.

Mwanasheria Maalum Jack Smith

Hatua hiyo imewaathiri karibu waendesha mashtaka kumi, ambao walikuwa kwenye kesi kuhusu namna Trump alizishughulikia nyaraka za siri na kesi ya kuingilia uchaguzi. Mwanasheria Maalum Jack Smith aliamua kuzitupilia mbali kesi zote mbili muda mfupi baada ya uchaguzi wa Desemba, akitaja sera ya Wizara ya Sheria inayokataza kumshtaki rais aliye madarakani.

Hii ilisababisha mjadala mkubwa kuhusu uadilifu wa sheria na namna kesi hizo zilivyoshughulikiwa. Jack Smith alijiuzulu mwishoni mwa muhula wa urais wa Biden, hatua ambayo imezua maswali zaidi juu ya uchunguzi huo na hatma yake.


Related Posts