RAIS SAMIA AMEFANYA MENGI YA MAENDELEO TUMUUNGE MKONO – RC MWASSA.

Mkuu wa Mkoa Kagera Hajat Fatma Mwassa amesema kuwa Wananchi na Wakazi wa Mkoa Kagera hawana budi kumpongeza na kumuombea Sana Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt Samia Suluhu Hassan kutokana na  shughuli nyingi za maendeleo zilizofanyika katika Mkoa huo.

Akizungumza wakati wa sherehe za kumpongeza Mhe. Rais Dkt. Samia kwa kutimiza Miaka 65 ya kuzaliwa, zilizoandaliwa na Umoja wa Wanawake wa CCM Mkoa wa Kagera (UWT), Hajat Fatma Mwassa amesema mengi yanaonekana yaliyofanywa na Dkt. Samia yakiwemo yanayohusu Elimu, Afya, Barabara, Maji, Bandari, huku mengine yakiwa yamekamilika na mengine yakiwa katika hatua za kukamilika na mengine yakianzishwa.

 “..kwa uchache mmeona Vituo vya Afya na Hospitali zimejengwa ni Kazi ya Mhe. Rais Dkt Samia, mmeona Shule nzuri na Watoto wetu wanasoma vizuri ni kazi ya Dkt Samia, Mmeona Bandari zetu za Bukoba na Kemondo kila moja zimeletwa Shilingi Bilioni 22   kazi inakamilika kufikia Mwezi Machi, Barabara Njia Nne zinajengwa ni Kazi ya Dkt. Samia, Maji, Barabara, Umeme mpaka Vitongojini ni mengine mengi ni kazi ya Mhe. Rais Samia..” amesema Hajat Mwassa.

Aidha ameongeza kuwa ni muda sasa wa Akina Mama hao wa CCM kuendelea kukiimarisha Chama Cha Mapinduzi kwa kumpambania Rais Dkt. Samia kuhakikisha anapata Ushindi wa kishindo katika Uchaguzi Mkuu wa Oktoba Mwaka huu, kwa kumtafutia Kura hadi chini ya Uvungu, na kuzilinda kura hizo, ili kumpa nafasi ya Miaka Mitano mingine akamilishe Miradi mingine ya Maendeleo.

Sherehe hizo za kumpongeza Rais Dkt Samia zimefanyika Kata Kashai Bukoba Manispaa na Kuhudhuliwa na Viongozi pamoja na Wanawake wa UWT kutoka Wilaya zote za Mkoa Kagera.

 

Related Posts