WANUFAIKA MPANGO WA TASAF UNGUJA WATOA SHUKRANI,WAFURAHIA MAFANIKIO

Na Mwandishi Wetu,Unguja

WANUFAIKA wa Mpango wa Maendeleo ya Jamii (Tasaf) wameushukuru mpango huo kwa kuwawezesha na kuwasaidia kuinua vipato vyao na familia zao kwa ujumla.

Wametoa pongezi hizo mbele ya wadau wa maendeleo walipotembelea baadhi ya wanufaika katika shehia ya Chumbuni Mkoa wa Mjini Magharibu Unguja.

Wakizungumza kuhusiana na mafanikio yao, baadhi ya wanufaika hao wamesema awali walikuwa wakiishi maisha ya kubangaiza lakini baada ya kuja mpango huo wa kunusuru kaya masikini wameinuka na kwasasa maisha yao yanaendelea kuneemeka.

Kupitia kipngele hicho walengwa wamepatiwa fursa za kuunda vikundi m na kupatiwa mafunzo ya stadi za maisha vinaendelea na shughuliza za uzalishaji zikiwemo ufugaji , kilimo cha mboga na baishara ndogondogo.

Mchunga Ali Mbigili amesema wakati anaingia kwenye mpango huo alikuwa akipata Sh36, 000 lakini kadri zilizvokuwa zinaendlea akawa maisha yake yaanzidi kumarika

Mwanamke huyo anayejishughulisha na ujasirimalia wa kushona nguo na mikoba, amesema alipata ruzuku ya Sh500,000 kisha akaazisha biashara hiyo na kwa siku anapata faida ya Sh20,000 ambayo anajiwekeza kwenye vikundi na kuweka akiba.

“Nimesomesha watoto wangu kwenye fedha hii, nasuka vikapu na kushna ngua, kwakweli nimehitimu kutroka kwenye mpango ila nashukuru tumepata faida kubwa na maisha yetu yameinuka

Mwingine, Keji Ali Juma, yeye amesema aliingia kwenye mpango akiwa anapata Sh61,000 lakini kwasasa amehitimu akiwa na mashine ya kuhoka mikate na keki ambayo amekuwa maarufu kwa ajili ya kuwatengenezea wananchi katika shehia hiyo.

“Mpango huu umenisaidia sana, kutoka kwenye kula mlo mmoja ahdi kula milo mitatu, tunaomba uendelee kuwasidia wengine amabo wanauhitaji nao waweze kusaidika katika maisha yao,” amesema

Mkurugenezi Mtendaji wa TASAF Shadrack Mziray amesema kwa kawaida wamekuwa na mapitio ya utekelezaji kila baada ya miezi sita hivyo wapo kwenye mapitio ya kawaida

“Amesema wanaeleeka katik akipindi cha mwisho kinachoishia Septemba mwaka huu, amesema

“Kikubwa tulichoona leo ni mafanikio makubwa ambayo yamepatikana kuzinyanyua kaya masikini, wengi wao waliotoka kwenye mpango ni wale ambao wamepewa ruzuku ya kila baada ya miezi mwili waliogezewa ya kuendeleza miradi yao ambayo ni wastani wa Sh350,000,” amesema

Amesema pamoja na programu hiyo licha ya kwenda ukingoni katika awamu ya pili, lakini wamekubaliana kwamba kuwe na programu nyigine ambayo ikianza kutekelezwa itachukua wale ambao hawakuwa kwenye program zilizioisha na inatarajia kuaza Septemba au Oktoba mwaka huo.

Nao wadau hao wa maendeleo kutoka Benki ya Dunia na ubalozi wa Ireland wameeleza jinsi walivyoridhishwa na mpango huo unavyotekelezwa baada ya kushuhudia simulizi mbalimbali za wanufaika hao.

Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Mkamu wa Pili wa Rais Zanzibar, Salhina Mwita Ameir amesema wananchi wanafarijika kwa miradi hiyo kama yalivyo malengo ya Tasaf yenyewe

“Kupunguza umasikini kuna njia nyingi, kuna kupunguza umasikini kupitia sekta ya elimu afya na fedha kwa kupata kipato pamoja na masula ya kimazingira yote lengo yake ni kuwawekea katika amzingira mazuri,” amesema.








Related Posts