Selina Gomez Afuta Video Aliyojirekodi Akilia – Global Publishers



 

Staa wa muziki na filamu duniani, Selena Gomez

 

Hapo jana, Jumanne ya Januari 28, 2025 staa wa muziki na filamu duniani, Selena Gomez alijirekodi video akiwa analia kisha akaipost kwenye akaunti yake ya Instagram, akiwalilia wahamiaji haramu ambao walikuwa wakirudishwa makwao baada ya amri ya Rais Donald Trump.

Muda mfupi baadaye, video hiyo ilikuwa gumzo duniani kote ambapo wapo waliompongeza lakini wafuasi wa Trump na wanachama wa Republican, hawakufurahishwa na video hiyo ambapo walianza kumshambulia Selena.

Baada ya kuona mambo ‘yamechemka’, Selena aliamua kuifuta video hiyo kutoka kwenye akaunti yake ya Instagram.

Taarifa kutoka kwa chanzo kilicho karibu na Selena, zinaeleza kuwa Selena hakutarajia kukutana na ‘zogo’ kubwa kiasi hicho mitandaoni, akaamua kufuta kwa sababu kwanza hakuwa anataka kuwapoteza wateja wa brand zake za urembo ambao ni wafuasi wa Trump.

Chanzo hicho kimeeleza kuwa, Selena ameahidi kutojihusisha tena na masuala ya kisiasa.

Miongoni mwa watu mashuhuri waliomshukia vikali Selena, ni Sam Parker aliyekuwa akiwania Useneta ambaye aliibuka na kudai kuwa msanii huyo naye ni mhamiaji na anapaswa kuondolewa nchini Marekani.


Related Posts