Bukombe. Mamia ya wakazi wa Wilaya ya Bukombe mkoani Geita wamejitokeza katika viwanja vya shule ya sekondari Businda kwa ajili ya kuwaaga wanafunzi saba waliopoteza maisha kwa kupigwa na radi Januari 27, 2025 wakiwa darasani wakiendelea na masomo, huku Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Dk Doto Biteko akiwa miongoni mwa waombolezaji.
Katika tukio hilo, wanafunzi wanne walifariki dunia papo hapo na wengine watatu walifariki dunia wakati wakipatiwa matibabu hospitali. Miongoni mwa waliofariki, wawili ni watoto pekee kwa wazazi wao.
Akisoma historia zao, Mwalimu Mkuu wa Shule ya Businda, Theodora Mushi amewataja watoto pekee kwa wazazi wao ni Peter Manyanda wa Bukombe na Erick Akonay, mzaliwa wa Arusha.
Katika ibada ya kuwaaga wanafunzi hayo, wapo viongozi mbalimbali akiwemo Naibu Waziri Mkuu, Doto Biteko, Mkuu wa Mkoa wa Geita, Martine Shigella na viongozi wengine.
Endelea kufuatilia mitandao ya Mwananchi kwa taarifa zaidi.