Mahakama Kuu yarejesha shauri la Dk Slaa Kisutu, yataka dhamana ipewe kipaumbele

Dar es Salaam. Mahakama Kuu Masjala ndogo ya Dar es Salaam imelirejesha shauri la mwanasiasa maarufu nchini, Dk Wilbrod Slaa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu huku ikiielekeza kulipa kipaumbele suala la dhamana yake.

Dk Slaa na jopo la mawakili wake walifungua shauri la mapitio la kesi yake katika Mahakama Kuu akipinga mwenendo wa Mahakama ya Kisutu kuahirisha usikilizwaji wa suala la dhamana yake kutokana na maombi ya kupinga dhamana yake yaliyotolewa na Jamhuri

Jaji Arnold Kirekiano leo Januari 30, 2025 amesema kwa kuwa kesi ya msingi iko Mahakama ya Kisutu ambayo ina mamlaka ya kusikiliza kesi hiyo na kwa kuwa hoja ya uhalali wa mashtaka ilishatolewa Kisutu na inasikilizwa na kupangiwa uamuzi amesema si vyema Mahakama Kuu kuingilia kati.

Hivyo Jaji Kirekiano ameelekeza Mahakama ya Kisutu itoe uamuzi ambao ilishauandaa.

Dk Slaa alikosa dhamana tangu alipopanda kizimbani Januari 10, 2025 kusomewa shitaka linalomkabili la kusambaza taarifa za uongo kupitia mtandao wa X.

Endelea kufuatilia Mwananchi

Related Posts