Matano atengeneza mtambo wa mabao Fountain Gate

KOCHA wa Fountain Gate, Mkenya Robert Matano amesema anatengeneza namna ya kuunganisha washambuliaji watatu nyota wa kikosi hicho katika michezo ya mzunguko huu wa pili, unaoanza kesho baada ya kupisha michuano ya Kombe la Mapinduzi.

Washambuliaji hao ni kinara wa ufungaji katika timu hiyo, Seleman Mwalimu aliyefunga mabao sita na Edgar William mwenye matano, sambamba na ingizo jipya la Mudrik Abdi Shehe ‘Gonda’ aliyejiunga nayo akitokea JKU SC kutoka visiwani Zanzibar.

Akizungumza na Mwanaspoti, Matano alisema moja ya mikakati yake ni kuhakikisha anatengeneza safu bora ya ushambuliaji kwa kuzingatia mahitaji ya timu hiyo, ingawa bado ana kazi kubwa pia ya kutengeneza balansi eneo lao lote la ulinzi.

“Nimekuwa na wiki tatu nzuri na nashukuru maendeleo ya timu sio mabaya sana kwa sababu tumepata michezo ya kirafiki na kwa hakika imenipa mwanga wa mambo ya kuanza nayo, wachezaji wote wameonyesha utayari jambo ambalo ni jema kwetu.”

Kocha huyo aliyewahi kuzifundisha timu mbalimbali zikiwemo za Sofapaka, Tusker FC zote za Kenya, alisema bado wachezaji wote hawajafikia katika kiwango anachokihitaji, ingawa wameanza kuelewa mifumo yake taratibu.

Mudrik Zanzibar alifunga mabao manane na ameongeza morali.

Related Posts