MCC RAJAB: UWEKEZAJI WA RAIS SAMIA KATIKA SEKTA YA ELIMU TANGA UMEWAOKOA WATOTO KUFANYISHWA KAZI ZA NDANI

MJUMBE wa Kamati Kuu ya Chama cha Mapinduzi (CCM) Taifa Rajab Abdurhaman amesema uwekezaji uliofanywa na Rais Dkt Samia Suluhu kwenye sekta ya elimu mkoani Tanga umesaidia kuwaokoa watoto kufanyishwa kazi za ndani.

Rajabu ambaye pia ni Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Tanga aliyasema hayo juzi wakati akizindua maadhimisho ya miaka 48 ya kuzaliwa chama hicho katika mkutano ulikuwa na lengo la kuunga mkono maamuzi ya mkutano mkuu maalumu wa CCM.

Maamuzi ya Mkutano Mkuu huo maalumu uliompitisha Dkt Samia Suluhu kuwa mgombea Urais, Dkt Emanuel Nchimbi kuwa mgombea mwenza pamoja na kumpitisha Stephen Wasira kuwa Makamu Mwenyekiti wa CCM Taifa uliofanyika kwenye eneo la Makorora Jijini Tanga.

Alisema hilo limetokana na uwekezaji wake kupitia elimu bure ambapo kwa mkoa wa Tanga kila mwezi kwa ada za watoto Rais anatoa Bilioni 1.3 kwa mwezi ambayo ni bilioni 15.8 kwa miaka.

“Kwa maana ya kipindi cha miaka mitano amewalipua watoto wetu bilioni 78,Rais asingelipa fedha hizo kwa ajili ya ada za watoto wetu kwa shule za msingi na sekondari ilipaswa kila mwanafunzi kulipiwa na mzazi “Alisema

Aidha alisema kutokana na kulipiwa ada za watoto maana yake amewasaidia baadhi ya majukumu kwenye familia ambazo zisingeweza kulia ada hiyo ndio sababu zilizopelekea mkutano mkuu kumpitisha kuwa mgombea urais 2025.

“Lakini niwaambie hapa kwamba CCM kupitia ilani Serikali kwenye suala la elimu ya msingi na sekondari imefanya kazi kubwa sana kwa kufanya uwekezaji mkubwa hivyo kuongeza ufaulu kwa darasa la saba, kidato cha nne na cha sita “Alisema

“Hivyo mtu anapohitaji msichana wa kazi na mvulani wa kazi utasakia nenda korogwe na Lushoto kwa sababu ya watoto wengi kufeli kutokana na kutokuwa na uwekezaji mkubwa kwenye elimu hivyo kutokana na uwekezaji wa Rais umesaidia kukua kwa elimu kupandisha ufaulu”Alisema

Aliongeza kwamba leo hii katika matokeo ya darasa la saba wasiofaulu ni wachache sana na wanakwenda kwenye vyuo vya ufundi na ndio maana kuwapata wasichana wa kazi au vijana huwezi kuwapata kwa sababu watoto wote wapo shuleni.

Hata hivyo Mwenyekiti huyo alisema kwamba wanaunga mkono azimio la mkutano mkuu wa CCM Taifa ambalo lilimpitisha Dkt Samia Suluhu kuwa mgombea Urais katika uchaguzi Mkuu mwaka 2025.

Alisema pia wanaunga mkono maamuzi kumpitisha Dkt Emanuel Nchimbi kuwa mgombea mwenza na Dkt Mwinyi kuwa mgombea Urais wa Zanzibar na wana Tanga wanaupongeza mkutano mkuu kwa kumchagua Stephen Wasira kuwa makamu CCM Taifa.

“Wapo wanaojiuliza kwanini mkutano Mkuu Mkuu Maalumu CCM umeamua kwa kura zote za wajumbe kumpitisha Dkt Samia Suluhu nimewahi kusema mara kadhaa tunapohitaji maendeleo ya kweli kwenye nchi na Taifa lipige hatua mbele za kimaendeleo jambo la kwanza unalohitaji ni amani.

“Niliwahi kuwaambia Tanga neno amani tunapenda kulidharau kwa sababu tumezoea kulitamka kila wakati unajua hata chakula unapokuwa unakula kila siku unafika wakati unakinai … watanzania neno hilo linahubiriwa misitiki na kanisani kila wakati inawezekana lakini tujifunze yaliyotokea na yanayotokea kwenye mataifa ya wenzetu barani Afrika na maeneo mengine duniani hvyo tuitunze amani yetu”Alisema

Related Posts