Meridianbet Yapeleka Msaada Zahanati ya Alimaua – Global Publishers


Katika kuendelea kuisadia jamii kwenye mahitaji mbalimbali, Meridianbet waliamua kufika katika zahanati ya Alimaua na kutoa msaada wa mashuka ambapo hii ikiwa ni mojawapo ya njia ya kurudisha kwa jamii.

Zoezi hilo la ambalo Meridianbet walifanya la kugawa mashuka katika Zahanati hiyo lina lengo la kuboresha mazingira ya utoaji wa huduma kwa wagonjwa na kusaidia wahudumu wa afya katika kazi zao za kila siku.

Katika zoezi hilo la kutoa msaada huo, Mwakilishi mkuu wa Meridianbeti Nancy Ingram alisema kuwa, “Tunajivunia sana kuwa sehemu ya mabadiliko chanya katika jamii hii. Huu ni mchango mdogo kutoka kwa kampuni yetu, lakini tunatumai kuwa utasaidia kuboresha mazingira ya huduma za afya katika Zahanati ya Alimaua. Tunajitahidi kutoa msaada kwa maeneo ambayo yana upungufu mkubwa na ambapo msaada wa haraka unahitajika. Kampuni yetu inajivunia kuchangia maendeleo ya jamii na tunatarajia kuendelea na juhudi hizi.”

Mwakilishi huyo pia aliendelea kusema kuwa Meridianbet itaendelea kuunga mkono miradi ya kijamii na afya kama sehemu ya dhamira yake ya kusaidia jamii inayoizunguka na kutimiza majukumu yake ya kijamii. Alisisitiza kuwa msaada wa mashuka ni sehemu ya mpango wa kudumu wa kampuni ya Meridianbet kusaidia na kuimarisha sekta za afya, elimu, na huduma za jamii.

Vilevile Meridianbet inakuambia hivi bashiri mechi za Europa leo uweze kupiga pesa sasa. Pia cheza michezo ya Kasino ya mtandaoni kama vile, Poker, Super Heli, Roullette, Aviator, Wild Icy Fruits, Keno na mingine kibao. Jisajili hapa.

Pia kwa upande wa Zahanati hiyo baada ya kupokea msaada huo wa mashuka walisema kuwa, “Tunashukuru sana kwa msaada huu kutoka kwa Meridianbet. Huu ni msaada muhimu kwa zahanati yetu na utasaidia kwa kiasi kikubwa katika kutoa huduma bora kwa wagonjwa. Mashuka haya yatasaidia sana katika kuimarisha mazingira ya kutolea huduma, hasa kwa wagonjwa wanaohitaji kulazwa. Tunashukuru kwa msaada wao na tunaomba kuwa juhudi hizi ziendelee.”

Meridianbet imeahidi kuendelea kurejesha kwenye jamii kwani uhitaji ni mkubwa sana ambapo kwa mwaka huu watajikita kwenye sekta mbalimbali ikiwemo, elimu, afya na zingine nyingi.

 

 

 

Related Posts