Kampala. Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Usalama wa Ndani la Uganda (ISO), Brigedia Jenerali Charles Oluka amefariki katika hospitali moja Kampala-Entebbe jana Jumatano Januari 29, 2025.
Naibu Katibu wa Habari katika Ofisi ya Rais nchini humo, Faruk Kirunda ameandika kwenye ukurasa wake wa X;
“Habari za kusikitisha zilizotufikia ni za kifo cha ghafla cha Brigedia Jenerali Charles Oluka. Alifariki katika Hospitali ya Seguku ambako alikimbizwa leo (Jumatano) jioni.”
Akiwa mkuu wa ujasusi nchini Uganda tangu 2020, kwa mujibu wa Daily Monitor, Oluka alibeba jukumu la kujenga upya sifa ya kitengo cha ujasusi nchini humo kutokana mazingira yaliyoachwa na mtangulizi wake, Kanali Kaka Bagyenda.
Oluka, ambaye Januari 2024 alipandishwa cheo na Rais Museveni kuwa Brigedia Jenerali, amefariki akiwa na umri wa miaka 57.
Endelea kufuatilia mitandao ya Mwananchi kwa taarifa zaidi.