STANBIC BANK TANZANIA YATOA WITO WA UWEKEZAJI KATIKA SEKTA YA NISHATI NA USHIRIKIANO WA KIKANDA KATIKA MKUTANO WA EA-ECS 2025

 

Stanbic Bank Tanzania inasisitiza dhamira yake ya kuimarisha uwekezaji katika sekta ya nishati na kuwezesha kifedha miundombinu muhimu wakati wa Mkutano wa 5 wa Ushirikiano wa Nishati Afrika Mashariki (EA-ECS) 2025 unaofanyika jijini Arusha.

· Mkutano huu ni jukwaa muhimu la kuhamasisha ushirikiano wa kikanda na kuimarisha mifumo ya nishati kwa lengo la kupanua upatikanaji wa nishati, kutumia vyanzo endelevu vya nishati, na kuchochea maendeleo ya viwanda.

· Stanbic Bank inaendelea kuwa mshirika muhimu katika kuendeleza sekta ya nishati Tanzania kwa kutoa suluhisho za kifedha zinazochochea ukuaji endelevu na ustahimilivu wa kiuchumi.

Kadri Afrika Mashariki inavyoelekea katika zama mpya za mageuzi ya sekta ya nishati, Tanzania inachukua nafasi ya muhimu katika kuunda mustakabali wa sekta hii katika kanda. Katika Mkutano wa 5 wa Ushirikiano wa Nishati Afrika Mashariki (EA-ECS) 2025, Stanbic Bank Tanzania imethibitisha dhamira yake ya kuwezesha uwekezaji, katika miundombinu muhimu, na kusaidia maendeleo ya viwanda kama vichocheo vya ukuaji wa uchumi.

Kaulimbiu ya EA-ECS 2025 ni “Kuwezesha Afrika Mashariki: Kufungua Uwezo wa Nishati wa Tanzania kwa Soko la Nishati la Kikanda,” hivyo mkutano huu unawakutanisha viongozi wa serikali, wawekezaji, na wataalamu wa sekta ya nishati ili kujadili suluhisho za kupanua upatikanaji wa nishati, kuunganisha vyanzo vya nishati endelevu, na kuimarisha ushirikiano wa kikanda. Tanzania inapojiimarisha kama kitovu cha nishati ndani ya Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC), uwekezaji katika usalama wa nishati, miundombinu, na mifumo bunifu ya uwezeshaji fedha utakuwa kichocheo muhimu katika kufanikisha maendeleo ya sekta hii.

Stanbic Bank Tanzania inatambua umuhimu wa uwezeshaji wa kifedha katika kuleta mabadiliko chanya katika sekta ya nishati. Kwa kutumia utaalamu wa Standard Bank Group. Benki ya Stanbic imekuwa na mchango mkubwa katika kubuni suluhisho za kifedha zinazopunguza uhatarishi katika uwekezaji, kuwezesha ushirikiano wa kimkakati, na kuharakisha maendeleo ya miradi mikubwa ya miundombinu. Benki imechangia katika miradi mikubwa ya nishati ikiwa ni pamoja na utafiti wa uchumi mkuu wa gesi asilia (LNG) nchini Tanzania. Nje ya mipaka ya Tanzania, Standard Bank Group imesaidia uwekezaji mkubwa katika sekta ya nishati barani Afrika, ikiwa ni pamoja na kufadhili mradi wa nishati upepo wa Seriti Green nchini Afrika Kusini, kupanua suluhisho za nishati mbadala kupitia CrossBoundary Energy, na kufanikisha uwezeshaji wa mradi wa nishati upepo wa Lake Turkana Wind Power nchini Kenya, ambao ni shamba kubwa zaidi la nishati upepo barani Afrika.

Akizungumza katika EA-ECS 2025, Joe Mwakanjuki, Makamu wa Rais, Nishati na Miundombinu, Stanbic Bank Tanzania, alisisitiza umuhimu wa uwekezaji makini katika miundombinu ya nishati ili kuchochea maendeleo endelevu. “Sekta ya nishati ni uti wa mgongo wa maendeleo ya viwanda na ukuaji wa uchumi wa Tanzania. Katika Benki ya Stanbic, tunatambua kuwa ufadhili wa kifedha ni chachu muhimu ya mageuzi haya. Dhamira yetu ni kutoa suluhisho za kifedha bunifu zinazovutia uwekezaji, kupanua upatikanaji wa nishati, na kusaidia maendeleo endelevu ya kiuchumi,” alisema.

Kushiriki kwa Benki ya Stanbic katika EA-ECS 2025 kunadhihirisha dhamira yake ya kusaidia ukuaji wa Tanzania kwa kushirikiana na taasisi za serikali, sekta binafsi, na wadau wa maendeleo ili kutatua changamoto za sekta ya nishati, kufungua fursa za uwekezaji, na kuimarisha nafasi ya Tanzania kama mchezaji muhimu katika soko la nishati la kikanda.

Kadri EA-ECS 2025 unavyoendelea kuweka mwelekeo wa mustakabali wa sekta ya nishati Afrika Mashariki, Stanbic Bank inasalia kuwa mshirika mkuu katika kuhakikisha kuwa dira ya Tanzania ya kuwa kituo cha nishati kikanda inatimia. Kupitia ushirikiano wa kimkakati, ufadhili bunifu, na dhamira ya muda mrefu kwa maendeleo endelevu, benki inalenga kuharakisha mabadiliko ya sekta ya nishati na kusaidia ustawi wa kiuchumi katika ukanda mzima.

Mkuu wa Kitengo cha Sekta ya Umma wa Benki ya Stanbic Tanzania, Noella Kimaro (kulia), akibadilishana mawazo na Tusekile Kibonde, Afisa Mwandamizi kutoka African Trade & Investment Development Insurance, wakati wa Mkutano wa tano wa Ushirikiano wa Nishati Afrika Mashariki (EA-ECS) 2025 unaofanyika jijini Arusha chini ya udhamini wa Benki ya Stanbic Tanzania.Ofisa Mwandamizi anayehusika na Nishati na Miundombinu wa Benki ya Stanbic Tanzania, Joe Mwakanjuki (wa pili kushoto), akibadilishana mawazo ya baadhi ya watoa wakati wa Mkutano wa tano wa Ushirikiano wa Nishati Afrika Mashariki (EA-ECS) 2025 unaofanyika jijini Arusha. Wanaomtazama kutoka kushoto ni Francois Xavier Dubois, Mkuu wa Maendeleo ya Biashara kwa Afrika Mashariki kutoka Siemens Energy, na Makamu wa Rais wa Taqa Arabia anayehusika na Afrika na Miradi Mipya, Adly Kafafy.

Naibu Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO), Mhandisi Costa Rubagumya (kushoto), akichangia mada wakati wa Mkutano wa tano wa Ushirikiano wa Nishati Afrika Mashariki (EA-ECS) 2025 unaofanyika jijini Arusha chini ya udhamini wa Benki ya Stanbic Tanzania.

Related Posts