Na Jane Edward,Arusha
Wadau mbalimbali wa sekta ya nishati wameelezea kufurahishwa kwao na mkutano wa sita wa wadau wa sekta ya nishati wa nchi nane za jumuiya Afrika Mashariki [EAECS]na kuahidi kuendelea kushirikiana na serikali katika kuhakikisha nchi zinaondokana na changamoto ya ukosefu wa nishati ya umeme wa uhakika.
Akizungumza na waandishi wa habari katika mahojiano maalumu katika mkutano wa EAECS unaomalizika leo jijini Arusha,Mkurugenzi mkaazi wa Tanzania kutoka shirika la Bima la uwekezaji biashara Afrika[ATIDI] Tusekile Kibonde amesema pamoja na kwamba shirika hilo ni kibiashara lakini bado wanaunga jitihada za serikali katika nyanja mbalimbali ikiwemo nishati ya umeme.
Kibonde amesema npaka sasa taasisi imewezesha zaidi ya dola Bilioni 1 katika miradi ya kimkakati ya maendeleo ya nchi ya Tanzania lengo likiwa ni kuhakikisha nchi inafikia malengo yake ya kimkakati ya maendeleo.
”mpaka sasa tuna miradi ambayo tumeigusa moja kwa moja ambayo ni reli,bandari,miundombinu ya barabara ikiwemo madaraja ,sekta ya afya pamoja na nishati ya umeme vijijini yani REA pamoja na sekta ya madini, kwahiyo tukikutana kwa pamoja kama hivi tunajadili na kujua namna ya kusaidia nchi”alisema Kibonde
Aidha amesema uwepo wa mkutano huo ni wadau wanaosaidia sekta hiyo kupiga hatua na kuleta unafuu wa upatikanaji wa umeme sanjari na kufanya mazungumzo nna shirika la umeme Tanzania ili kuweza kukubaliana maeneo gani ya kuwekeza.
Kwa upande wake muwakilishi wa vijana bunge la Afrika mashariki Silvesta Magesa amesema uwepo wa soko huru la nishati ya umeme umeme inasaidia nchi wanachama kupata umeme kwa gharama nafuu ili kukuza uchumi wa mtu mmoja mmoja.
Amesema kupitia mkutano huo kila nchi ihakikishe inaongeza uzalishaji wa nishati mbadala badala ya kutegemmea chanzo kimoja tu hali itakayosaidia kuacha kutegemea misaada kutoka nje kwani uzalishaji wa viwanja vinategemea uwepo wa umeme wa uhakika.
”soko la pamoja la afrika mashariki inasaidia nchi zilizopo katika umoja huo katika kupunguza gharama badala yake watumie vyanzo mbadala ili kupunguza ukosefu wa nishati ya umeme kwa nchi hizo”Alisema Magesa
MWISHO…………..