Rais wa Marekani, Donald Trump amesema mgogoro unaoendelea kati ya Rwanda na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo ni tatizo kubwa.
Akizungumza katika mkutano wake na waandishi wa habari kuhusu ajali ya ndege jijini Washington, Trump aliulizwa na mwandishi mmoja wa habari aliyetaka kujua kama Marekani ina mpango wa kwenda kurudisha amani Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo.
Akijibu swali hilo, Trump alisema:
“Unaniuliza kuhusu Rwanda, ni tatizo kubwa sana, nakubaliana na wewe lakini sidhani kama ni sahihi kwa sasa kulizungumzia jambo hilo. Lakini ni tatizo kubwa sana,” alisema.
Rwanda imekuwa ikituhumiwa kuchochea machafuko Mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo kwa kuwaunga mkono M23 lakini Rais Paul Kagame amekuwa akikanusha tuhuma hizo.