Watanzania nchini wametakiwa kujenga tabia ya kuwasaidia watu wenye uhitaji maalum ikiwemo Watoto yatima Wazee Pamoja na watu wenye ulemavu ili waweze kuwa na furaha katika Maisha yao.
Wito huo umetolewa leo na Sheikh Mkuu wa Wilaya ya Ubungo Salumu Kidebe kwenye hafla fupi ya kumpongeza Dkt.Said Lugumi kwa sala na Dua maalumu ikiwa ni chachu ya kuwatia moyo wale wote wanaofanya mambo mema ya kijamii iliyofanyika katika Kata ya Msigani wilayani humo.
Pia Shekh kidebe amewataka wananchi kuwa mstari wa mbele kuwapongeza watu wote ambao wanafanya mambo ya heri katika jamii ya kuwasaidia watu wenye uhitaji maalumu
Kwa Upande wake Muandaaji wa hafla hiyo Watende Kiyagi,ambaye pia ni Mkurugenzi wa Kampuni ya W Printing Solution amesema katika Maisha yake amewahi kupitia changamoto nyingi hivyo anajua uchungu na maumivu ya watu wenye uhitaji hivyo kitendo alicho kifanya Dkt.Lugumi cha kusaidia Watoto yatima kimewapa furaha Watoto hao ndiyo maana akaamua kumuombea dua na kumpongeza kwa kitendo hicho.
Amesema kwa dunia ya leo mitandaoni kumekuwa Habari nyingi zisizo za muhimu lakini ndiyo zinapewa kipaumbele zaidi kuliko za watu ambao wamekuwa wakifanya kazi kubwa ya kusaidia jamii .
Naye Diwani wa kata ya Msigani Hassan Mwasha amempongeza muandaaji wa tukio hilo kwa sababu jambo alilolifanya Dkt Lugumi siyo la kulikalia kimya linahitaji pongezi kwa sababu wapo watu ambao wanamali nyingi lakini ni vigumu sana kuwaona wakijitoa pale ambapo kunauhitaji wa kujitoa katika jamii.