37 wateuliwa kamati za kudumu Coastal Union

MWENYEKITI wa Klabu ya Coastal Union, Muhsin Ramadhan Hassan, ameteua Kamati za Kudumu klabuni hapo ikiwa zimepita takribani siku 40 tangu uongozi mpya uingie madarakani.

Hassan ambaye alichanguliwa kuwa mwenyekiti wa klabu hiyo katika uchaguzi uliofanyika Desemba 23, 2024, ameteua kamati sita tofauti zinazoundwa na jumla ya watu 37.

Kamati ya fedha, mipango na rasimali itakuwa na mwenyekiti Dkt. Fungo Ally na wajumbe wake Abeid Mfaume, Nassoro Mohamed, Ahmed Menye, Bakar Fumbwe, Bwana Chambo, Abdi Masamaki, Saidi Bandawe na Omari Kombo.

New Content Item (2)
New Content Item (2)

Kamati ya Ufundi itakuwa chini ya Mwenyekiti Abdulrahman Fumbwe na wajumbe wake, Salim Omari, Razack Yussuf, Douglas Mhani, Abdallah Sabebe, Hassan Matan na Abdallah Bamzaku.

Upande wa Habari, Masoko na Udhamini Ally Sechonge ndiye mwenyekiti huku akisaidiwa na wajumbe wake Nassoro Mohamed, Abbas El Sabry, Thabit Abuu, All Hussein Kingazi na Bakari M Bakari.

Kamati ya Usajili itaongozwa na mwenyekiti, Mohamed Kiruwasha, wajumbe Abdallah Satelite, Emmanuel Mchechu, Khalid Abdallah na Hamis Salehe.

Kwenye nidhamu na maadili Unda Lugano ataongoza kama mwenyekiti huku wajumbe wake Hamis Karim, Said George, Hussein Moor na Shekuwe Pashua. Mwisho ni kamati ya Hamasa itaongozwa na Abdallah Unenge na wajumbe Saida Bawaziri, Jonathan Titto, Salim Bawaziri na Bwana Kitwana.

Related Posts