Ajali Nyingine Ya Ndege Marekani Yalipuka Angani – Global Publishers



Ndege ndogo ya matibabu aina ya jet, iliyokuwa ikimbeba mtoto mgonjwa, mama yake, na watu wengine wanne, ilianguka katika kitongoji cha Philadelphia, Marekani, muda mfupi baada ya kupaa. Ndege hiyo ililipuka angani na kusababisha mlipuko mkubwa wa moto ulioteketeza nyumba kadhaa katika eneo ilipoangukia, usiku wa kuamkia leo Jumamosi Feb 2025.

Kampuni ya Jet Rescue Air Ambulance, iliyokuwa ikiendesha ndege hiyo aina ya Learjet 55, ilitoa taarifa ikisema: “Hatuwezi kuthibitisha kama kuna manusura.” Hakukuwa na taarifa za haraka kuhusu iwapo mtu yeyote aliyekuwa ardhini alipoteza maisha.

Abiria wote sita waliokuwamo ndani ya ndege hiyo walitokea Mexico. Kwa mujibu wa msemaji wa Jet Rescue, Shai Gold, mtoto huyo alikuwa akipokea matibabu mjini Philadelphia na alikuwa akisafirishwa kurejea nyumbani.

Mtoto mgonjwa na mama yake walikuwa wakisafiri pamoja na wahudumu wanne wa ndege. Gold alieleza kuwa wahudumu hao walikuwa na uzoefu mkubwa, na kila mtu anayehusika na safari za aina hii hupitia mafunzo ya kina.

“Tukio kama hili linapotokea, ni jambo la kushangaza na kushtua,” Gold aliambia Shirika la Habari la Associated Press. “Ndege zote zinatunzwa kwa umakini mkubwa, hakuna hata senti moja inayopunguzwa, kwa sababu tunafahamu umuhimu wa kazi yetu.”











Related Posts