JAFO AZINDUA MFUMO WA KUTUMIA KAMERA ZA KIDIGITALI NA STIKA YA UTAMBUZI WA GHALA

WAZIRI wa Viwanda na Biashara,Mhe.Dkt.Selemani Jafo,akiangalia mfumo unavyofanya kazi mara baada ya kuzindua Mfumo wa kutumia kamera za kidijitali na stika ya utambuzi wa ghala,hafla iliyofanyika leo Januari 31,2025 jijini Dodoma

Na.Mwandishi Wetu-DODOMA

WAZIRI wa Viwanda na Biashara,Mhe.Dkt.Selemani Jafo ameitaka Bodi ya Usimamizi na Stakabadhi za Ghala kuusimamia Mfumo wa kutumia kamera za kidijitali na stika ya utambuzi wa ghala ili wanunuzi waweze kuuamini huku akiwataka watumishi wa Taasisi hiyo kuacha alama katika utendaji kazi wao.

Dkt.Jafo ametoa kauli hiyo leo Januari 31,2025,Jijini Dodoma wakati akizungumza katika Uzinduzi wa Mfumo wa kutumia kamera za kidijitali na stika ya utambuzi wa ghala.

Waziri Jafo ametaka Mfumo huo uwe imara ili kuongeza uaminifu kwa wateja na kuweza kuona Kila kitu kilichopo katika ghala lako.

“Mkurugenzi (Asangye Bangu) huu mfumo uwe imara tutengeneze kujiamini kwa wanunuzi na tuwatafute vijana wa tehama, Mteja atachokiona ndio kiwe uhalisia hatutaki ukanjanja…mmefanya jambo kubwa.Mtaendelea kufanya ubunifu imani kubwa mtafanya connection nzuri.Mimi sina mashaka na jinsi mnavyoenda,”amesema Waziri Jafo

Hata hivyo,Dkt. Jafo ameipongeza Taasisi hiyo kwa kufanya vizuri pamoja na kukutana na changamoto mbalimbali kwani inaashiria utendaji kazi mzuri.

“Wakulima walikuwa wanasema Mbaazi hainunuliki lakini kupitia Mfumo wa Stakabadhi ghalani umefanya vizuri,Mkurugenzi Mtendaji Bangu nakupa maua yako mmefanya vizuri.

Amesema kipindi cha nyuma korosho zilichanganywa na mawe kupelekea kutaka kuharibu soko la zao hilo nje lakini Sasa hivi mambo yanaenda vizuri.

Amesema kupitia Mfumo huo mnunuzi anaweza kuona hata akiwa nje ya Tanzania.

Dkt.Jafo amewaomba wale wanaosimamia maghala kuweka logo ili Mfumo huo uweze kufanya vizuri zaidi.

Kuhusu watendaji wa Serikali,Dkt.Jafo amewataka kuendelea kufanya vizuri zaidi huku akaigiza Kila mtumishi kufanya kazi kwa bidii ili kuacha alama.

“Niwaambie muda tunautumia katika kazi leo kuna mtumishi anaomba likizo siku 28 weka mashaka kama atakukubalia,tengenezeni Utamaduni kazi zinaenda vizuri.Imani ya gu Kila mmoja atatimiza wajibu wake.

“Fanya kazi acha legacy hakikisha mtu anaekuja kiatu kisimtoshe.Fanya kazi kama ni ibada.Fanyeni kazi tulete mabadiliko,”amesema Waziri Jafo.

Kwa upande wake Mkurugenzi Mtendaji wa Bodi ya Usimamizi wa Stakabadhi za Ghala,Bw.Asangye Bangu,amesema kazi yao kubwa ni kuwezesha biashara pamoja na kutoa leseni huku akidai sababu ya uwepo wao ni kurasimisha masoko,kuwezesha wakulima kulipwa vizuri,kuongeza ubora na hivyo kuongezeka kipato kwa watanzania.

Amesema mwaka huu wameshuhudia ongezeko la mapato katika mazao yanayotumia Mfumo.

Amesema wamejipanga na Wizara ya mifugo kuingiza zao la Mwani na samaki pamoja na Madini katika Mfumo huo.

“Nikuhakikishie tumesimama imara na tunaendelea kutekeleza kwa ufasaha.Maelekezo yako tutayafanyia kazi na kuyapokea,”amesema Bw. Bangu

Naye Meneja Uratibu na Huduma kutoka Bodi ya Usimamizi wa Stakabadhi za Ghala Bw.Abubakari Ndwata,amesema stika ya utambuzi kazi yake ni kutoa taarifa,jina la ghala,umiliki,mahali lilipo,mtu anaweza kuingia ndani ya ghala ili aweze kuona,zao kwa wakati huo,kiasi cha mzigo,idadi ya magunia na uzito wa magunia.

“Nembo hii ya utambuzi inaenda kuongeza uaminifu wetu ili wanunuzi wawe wanajiamini,Mheshimiwa Waziri Jafo umeona tumeuza korosho nyingi,”amesema Bw.Ndwata

WAZIRI wa Viwanda na Biashara,Mhe.Dkt.Selemani Jafo,akizungumza wakati akizindua Mfumo wa kutumia kamera za kidijitali na stika ya utambuzi wa ghala,hafla iliyofanyika leo Januari 31,2025 jijini Dodoma.

MKUU wa Mkoa wa Dodoma Mhe.Rosemary Senyamule,akitoa salamu za Mkoa wake wakati wa hafla ya uzinduzi wa Mfumo wa kutumia kamera za kidijitali na stika ya utambuzi wa ghala, leo Januari 31,2025 jijini Dodoma.

MKURUGENZI Mtendaji wa Bodi ya Usimamizi wa Stakabadhi za Ghala,Bw.Asangye Bangu,akielezea jinsi walivyojipanga na Mfumo wa kutumia kamera za kidijitali na stika ya utambuzi wa ghala,wakati wa hafla iliyofanyika leo Januari 31,2025 jijini Dodoma.

MKUU wa Chuo cha Elimu ya Biashara (CBE), Prof. Edda Tandi Lwoga, wakati wa hafla ya uzinduzi wa Mfumo wa kutumia kamera za kidijitali na stika ya utambuzi wa ghala, leo Januari 31,2025 jijini Dodoma.

Meneja Uratibu na Huduma kutoka Bodi ya Usimamizi wa Stakabadhi za Ghala Bw.Abubakari Ndwata,akielezea jinsi mfumo huo utakavyokuwa unafanya kazi wakati wa hafla ya uzinduzi wa Mfumo wa kutumia kamera za kidijitali na stika ya utambuzi wa ghala, leo Januari 31,2025 jijini Dodoma.

WAZIRI wa Viwanda na Biashara,Mhe.Dkt.Selemani Jafo,akizundua Mfumo wa kutumia kamera za kidijitali na stika ya utambuzi wa ghala,hafla iliyofanyika leo Januari 31,2025 jijini Dodoma.

WAZIRI wa Viwanda na Biashara,Mhe.Dkt.Selemani Jafo,akiangalia mfumo unavyofanya kazi mara baada ya kuzindua Mfumo wa kutumia kamera za kidijitali na stika ya utambuzi wa ghala,hafla iliyofanyika leo Januari 31,2025 jijini Dodoma.

Related Posts