Mwanadada aliyewahi kujihusisha na sanaa ya Bongo Muvi, Carolinahawa Hussein, kwa mara nyingine tena anakabiliwa na tatizo la utumbo wake kutoboka na kuanza kumwaga uchafu wa haja kubwa kupitia mshono wake.
Hali hii imetokea mwezi mmoja tu baada ya kufanyiwa upasuaji wa mara ya 24, ambao ulifanyika haraka kutokana na utumbo wake kutoboka.
Kwa majonzi makubwa, Carina alieleza hali yake akisema:
“Mimi nimekata tamaa. Nilidhani safari hii ningepata nafuu kwa sababu nilikuwa naanza hata kutoka nje kidogo na kufanya kazi za mikono. Lakini kumbe sivyo. Jana usiku mshono wangu ulianza kuvuja tena choo, jamani… nimekata tamaa,” alisema huku akilia kwa uchungu.
Carina amekuwa akiteseka na hali hii kwa takribani miaka minane. Kwa sasa, madaktari wamemshauri aende India kwa matibabu maalum, lakini ukosefu wa fedha umekuwa kikwazo kikubwa. Kila mara anapopata msaada wa kifedha, unatumika kwa upasuaji wa dharura hapa nchini, hali inayomfanya kushindwa kusafiri kwa matibabu sahihi.
Ikiwa umeguswa na hali ya Carina, unaweza kumchangia kupitia:
Mpesa: 0769990045 (Carolinahawa Hussein Ebrahim Bounin)
Tigopesa: 0712595858 (Carolinahawa Hussein Ebrahim Bounin)