Msajili Mkuu wa Mahakama ya Tanzania, Mhe. Eva Kiaki Nkya, amezitaka taasisi zilizopo kwenye mnyororo wa haki jinai kuendelea kushirikiana ili kutoa haki kwa wakati kwani miongoni mwa nguzo muhimu za mafanikio ni ushirikiano
Nkya ameyasema hayo wakati akifunga maonesho ya wiki ya Sheria kitaifa katika viwanja vya Nyerere Square jijini Dodoma Februari 1, 2025, ambapo amezishukuru Taasisi zote zilizoshiriki katika maonesho hayo huku akizitaka kuendeleza ushirikiano huo ili kuongeza ufanisi kwenye upatikanaji wa haki jinai
“Nawashukuru Washiriki wote na wadau wote walioshiriki ninyi ndio chachu ya mafanikio ya wiki ya Sheria ambapo Mahakama tumeshirikiana na wadau wetu kutoa elimu ya Sheria na Haki katika Mabanda na kuwafuata wananchi waliko, na Kupitia kuwafuata wananchi kwenye shughuli zao imesaidia kuwafikia wananchi wengi zaidi, ikiwa ni kutekeleza mpango wa nguzo ya tatu ya Mahakama ambao unazungumzia kushirikiana na wadau wengine ili kufanikisha kwa ufanisi utoaji elimu ya upatikanaji wa haki” alisema Nkya
Mwenyekiti wa Kamati ya Maandalizi ya Maonesho hayo ambaye ni Msajili wa Mahakama ya Rufani, Mhe. George Herbert, amesema maonesho ya mwaka huu yamefanikiwa kuwafikia wananchi wengi zaidi ndani na nje ya mabanda
“Tulikuwa na Taasisi 39 na jumla ya wananchi 3446 wametembelea mabanda ili kupata elimu ya Sheria haki na utatuzi wa migogoro mbalimbali huku idadi nyingine tumeifikia kwa njia ya vyombo vya habari” alisema George.
Akitoa salam za Shukrani kwa niaba ya Taasisi zote zilizoshiriki katika maonesho hayo, Mkurugenzi wa Huduma za Sayansi Jinai kutoka Mamlaka ya Maabara ya Mkemia Mkuu wa Serikali, David Elias, amesema Taasisi zimeshiriki maonesho hayo kwa lengo la kutoa elimu ya maswala ya haki na kutatua changamoto za wananchi.
“Tumeshiriki maonesho haya kikamilifu tukijikita katika kutoa elimu na kuwahudumia watanzania kupitia miondombinu tuliyowezeshwa na Serikali ya awamu ya sita chini ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan, na kama maono yake yalivyo kuelekea Dira ya Taifa 2050 mifumo isomane kupitia teknolojia na Tehama” alisema Elias.
Msajili Mkuu wa Mahakama ya Tanzania, Mhe. Eva Kiaki Nkya (kulia) akimkabidhi cheti cha ushiriki Mkurugenzi wa Huduma za Sayansi Jinai wa Mamlaka ya Maabara ya Mkemia Mkuu wa Serikali, David Elias (kushoto) wakati akifunga maonesho ya wiki ya Sheria katika viwanja vya Nyerere Square jijini Dodoma Februari 1, 2025. Katikati ni Msajili wa Mahakama ya Rufani, George Herbert.
Mkurugenzi wa Huduma za Sayansi Jinai, David Elias, akitoa neno la shukrani kwa niaba ya Taasisi zote zilizoshiriki maonesho ya wiki ya sheria wakati wa kufunga maonesho ya wiki ya Sheria katika viwanja vya Nyerere Square jijini Dodoma Februari 1, 2025.
Mkuu wa Wilaya ya Dodoma Mjini, Jabir Shekimweri (kulia) akisikiliza maelezo kutoka kwa mtumishi wa Mamlaka, Sadock Mboya (kushoto) juu ya majukumu la Mamlaka ya Maabara ya Mkemia Mkuu wa Serikali kwenye mnyororo wa Haki jinai, wakati alipotembelea banda la Mamlaka kwenye maonesho ya wiki ya Sheria katika viwanja vya Nyerere Square jijini Dodoma.
Mkurugenzi