NMB YATOA ZAWADI MIL200 KWA WATEJA WAKE KUPITIA DROO YA MASTABATA

Na Khadija Kalili
Michuzi TV
Benki ya NMB jana imetoa zawadi pesa zenye thamani ya Mil.200 kwa washindi zaidi ya 1,700 kupitia promosheni ya Mastabata.
Akizungumza katika mkutano uliofanyika tarehe 30, 2025 katika Ofisi za NMB Bagamoyo Mkoani Pwani Meneja Huduma wa tawi hilo Mapesa Agrey Mapesa amesema kuwa huu ni msimu wa sita wa promosheni hiyo ya Mastabata.
Msimu huu wa sita promosheni ya Mastabata ya kibabe imedumu kwa miezi mitatu huku washindi zaidi ya 2,000 wamepatikana” amesema Mapesa.
Katika fainali ya droo ambayo tumepanga ifanyike tarehe 12 Februari 2025 tunatarajia kutoa zawadi zenye thamani ya Mil.300 pia kupata washindi watano ambao watagharamiwa na Benki ya NMB kwenda mbungani kuona wanyama na wenza wao huku wakilipiwa gharama zote kula kulala na mengineyo” amesema Mapesa.
Washindi wengine watano watajishindia kiasi cha Mil.4 kila mmoja ambazo zitakua kwa ajili ya kuwalipia ada watoto wao ama kwa matumizi binafsi” amesema Meneja huyo wa Tawi la NMB Bagamoyo.
Katika droo hiyo imekua ikitoa zawadi ya fedha taslimu kiasi cha Sh.100,000 papo kwa hapo kwa washindi 40 kila wiki.

Related Posts