Makamu Mwenyekiti wa Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi Mhe. Jahi (Rufaa) Mbarouk S. Mbarouk.
Chifu wa Mkoa wa Pwani Salim Mashimb
Na Khadija Kalili Michuzi TV
MAKAMU Mwenyekiti wa Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi Mhe.Jaji (Rufaa) Mbarouk S. Mbarouk amesema wananchi wanatakiwa kujitokeza kuboresha taarifa zao kwenye daftari la mpigakura ndani ya siku saba ambapo ni kuanzia Februari 13 hadi 19 2025 na vituo vitakuwa vinafunguliwa kuanzia saa mbili asubuhi na kufungwa saa 12 jioni.
Mhe.Jaji Mbarouk amesema hayo leo tarehe 1 Februari 2025 kwenye mkutano na wadau wa uchaguzi kuhusu uboreshaji wa daftari la kudumu la wapiga kura kwenye mkutano uliofanyika katika Ukumbi wa Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Pwani.
“Tume katika kuhakikisha inakwenda sambamba na na mabadiliko ya teknolojia ikiwa ninpamoja na kurahisisha zoezi hili uboreshaji wa daftari,imeboresha mfumo wa uandikishaji ambao mara ya kwanza utamuwezesha mpiga kura aliyepo kwenye daftari kuanzisha mchakato wa kuboresha taarifa zake au kuhama kituo kwa kutumia aina yeyote yq simu ya kiganjani au kompyuta” amesema Mbarouk.
Amesema kuwa anawakumbusha wadau na wananchi kwamba kujiandikisha kuwa mpiga kura zaidi ya mara moja ni kosa la jinai kwa kuzingatia masharti ya kifungu cha 114(1) cha Sheria ya Uchaguzi wa Rais,Wabunge na Madiwani Na.1 ya mwaka 2024.
Amesema kifungu hicho kinaeleza kuwa mtu yeyote atakayeomba kuandikishwa zaidi ya mara moja atakuwa ametenda kosa la jinai nanakitiwa hatiani adhabu yake ni faini isiyopungua miezi sita jela na kisichozidi miaka miwili gerezani au vyote kwa pamoja yaani kulipa faini na kifungo gerezani.
Amesema kuwa wadau mliopo haoa nendeni mkawaelimishe wananchi kwamba wakajiandikishe mara moja kwenye Kituo kimoja ili kuepuka uvunjaji wa sheria.
“Kwa kuzingatia masharti ya kifungu ya kifungu cha 168 cha Sheria ya Uchaguzi wa Rais ,Wabunge na Madiwani Na.1 ya mwaka 2024 kadi za mpiga kura zilizotolewa mwaka 2015 na 2020 zenye jina la Tume ya Taia ya Uchaguzi ni halali na zitaendelea kutumika kwenye chaguzi zijazo.
“Zoezi hili la uboresha wa Daftari haliwahusu wapiga kura wenye kadi hizo na ambao kadi zao hazijaharibika au kupotea au hawajahama kutoka eneo moja la uchaguzi kwenda eneo jingine au taarifa zao hazijakosewa au hawahitaji kuboresha taarifa zao.
Amesema kuwa Tume imeweka utaratibu kwa watu wenye ulemavu ,wazee, wagonjwa,wajawazito na wakina mama wenye watoto wachanga watakaokwenda nao vituoni kupewa fursa ya kuhudumiwa bila kupanga foleni,tunawaomba wadau wa uchaguzi muwafahamishe wananchi wote waliopo kwenye makundi tajwa kujitokeza kwa wingi kwenda kujiandikisha au kuboresha taarifa zao vituoni kwa kuwa kumewekwa utaratibu mzuri wa kuwahudumia” amesema Mhe. Mbarouk.
Amesema kuwa kila Chama Cha Siasa kimepewa nakala ya orodha vituo vyote vya kuandikisha wapiga kura huku dhumuni la kuwapatia nakala hizo ni kuwawezesha kupanga na kuweka mawakala wa uandikishaji katika vituo vya kuandikisha wapiga kura.
Imeelezwa kuwa kila Chama Cha Siasa kitaruhusiwa kisheria kuweka wakala mmoja kwenye Kituo cha kuandikisha wapiga kura kwa lengo la kushuhudia utekelezaji wa zoezi la uboreshaji kituoni ikiwemo kuwatambua wale wanaokuja Kituoni kama wana sifa za kuandikishwa.
“Mawakala au Viongozi wa Vyama vya Siasa hawaruhusiwi kuingilia mchakato wa uboreshaji wa Daftari la Kudumu la Mpigakura Kituo ni hivyo nawaomba Viongozi wa Vyama Siasa na wadau wa uchaguzi kwa ujumla kuzingatia Sheria ya Uchaguzi, Kanuni, za Uboreshaji na maelekezo ya Tume na kusimamia miiko na mipaka ya uendeshaji wa zoezi la uboreshaji wa Daftari.
Kauli mbiu ya uboreshaji wa Daftari la Kudumu la Wapiga Kura kwa mwaka 2024/25 inasema Kujiandikisha kuwa Mpiga Kura ni Msingi wa Uchaguzi.