VIONGOZI FANYENI KAZI KWA USHIRIKIANO ILI KUYAFIKIA MAENDELEO – NGEZE

Na Dulla Uwezo

Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Bukoba na Diwani wa Kata ya Rukoma Murshid Ngeze amesema kuwa Viongozi ngazi za Kata, Vijiji na Vitongoji hawana budi kufanya kazi kwa kushirikiana na kupendana ili kuyafikia maendeleo yaliyokusudiwa.

Mhe. Ngeze ambaye pia ni MwenyeKiti wa ALAT Taifa akiwaongoza Wenyeviti na Mameya wote Tanzania, ametoa wito huo akiwa katika Ziara ya Siku moja Katika Kata za Kibirizi na Rukoma alipotembelea Kata hizo kukagua Mradi wa Ujenzi wa Zahanati ya Kibirizi pamoja na kusikiliza Kero Januari 31, Mwaka huu.

Kwa nyakati tofauti Mhe. Ngeze amenukuliwa akiwaasa Viongozi hao kuishi katika Misingi ya Ushirikiano na mshikamano akiwapitisha kwenye mifano mbalimbali ambayo itawasaidia kuyafikia maendeleo, hasa kwa kipindi hiki ambacho Taifa linaelekea kuwa na Uchaguzi Mkuu Oktoba 2025.

Awali akiwa Katika Kata ya Kibirizi Mhe. Ngeze amepata nafasi ya kusikiliza baadhi ya changamoto za Wananchi hao ikiwemo changamoto ya maeneo korofi barabara,

na kisha akatembelea na kujionea Zahanati ya Kata hiyo ambayo Ujenzi wake umefikia hatua ya kupaua.

Wakazi wa Kata hiyo wanadai kuwa wamekuwa wakifuata huduma za afya Umbali mrefu jambo ambalo limekuwa likiwapa usumbufu mkubwa na hasa nyakati za Mvua, na wakati mwingine Wajawazito hulazimika kujifungulia Barabarani, hivyo Zahanati yao itakapokamilika ambayo pia imechangiwa na Nguvu za Wananchi pamoja na Mbunge, itakuwa ni mkombozi na msaada mkubwa kunusuru maisha yao.



Related Posts