Aziz KI wa Yanga SC Princess nje wiki nne

MSHAMBULIAJI wa Yanga Princess, Ariet Udong anayefananishwa na nyota wa Yanga, Aziz KI atakuwa nje ya uwanja kwa miezi minne akiuguza majeraha ya mguu.

Nyota huyo mara ya mwisho kuonekana uwanjani ilikuwa Desemba 31 kwenye mzunguko wa nane wa Ligi akifunga mabao matatu dhidi ya Ceasiaa Queens ya Iringa.

Akizungumza na Mwanaspoti, kocha wa Yanga Edna Lema ‘Mourinho’ alisema kwa mujibu wa chumba cha madaktari mchezaji huyo atakuwa nje ya uwanja kwa wiki nne hadi tano.

“Madaktari wamesema atakuwa nje wiki nne kwa maana ya mwezi na tunamuombe apone haraka na kurudi kuisaidia timu,” alisema Mourinho na kuongeza:

“Sio pigo kubwa sana ingawa kila mchezaji ana umuhimu wake, naamini atarudi mapema lakini tunashukuru sasa yupo mbadala wake Jeaninne ambaye ameanza vizuri kwenye ligi.”

Akizungumzia mwenendo wa timu hiyo, alisema: “Duru la kwanza hatukuanza vizuri kwenye mechi mbili, lakini tumerejea na ushindi mzunguko wa pili naamini tutakuwa na muendelezo mzuri licha ya ugumu wa ligi.”

Related Posts