Clara Luvanga avunja rekodi yake Saudia

MSHAMBULIAJI wa Al Nassr inayoshiriki Ligi ya Wanawake nchini Saudia, Clara Luvanga amevunja rekodi ya msimu uliopita wa kufunga mabao 12.

Kwa sasa ndiye mshambuliaji tegemeo wa timu hiyo ambayo kwa upande wa wanaume yupo staa wa Ureno Cristiano Ronaldo.

Hadi sasa mshambuliaji huyo wa zamani wa Yanga amefunga hat-trick mbili — moja dhidi ya Al Ula na Eastern Flames, chama la zamani la Mtanzania mwenzake Enekia Lunyamila.

Msimu uliopita Luvanga alimaliza msimu na mabao 11 akimaliza kinara wa mabao kwa upande wa Al Nassr.

Huenda msimu huu ukawa bora zaidi kwa Luvanga ambaye anatazamwa kama Ronaldo wa kike kwenye klabu hiyo.

Zikiwa zimechezwa mechi 13 za Ligi hiyo na mabingwa hao watetezi wako kileleni na pointi 39.

Related Posts