UJENZI WA KITUO KIPYA CHA AFYA VUNTA JIMBO LA SAME MASHARIKI WAANZA RASMI.


NA WILLIUM PAUL, SAME.

WANANCHI wa kata za Vunta, Kirangare na Bwambo Tarafa ya Mamba Vunta katika Jimbo la Same mashariki wilayani Same mkoani Kilimanjaro waliokuwa wakitembea umbali wa kilomita zaidi ya 37 kufuata huduma ya Afya kituo cha Afya Miamba wataondokana na adha hiyo baada ya serikali kwanza ujenzi wa kituo kipya cha Afya Vunta.


Wananchi hao ambao wameonyesha shangwe kubwa kwa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan na Mbunge wa jimbo hilo, Anne Kilango Malecela baada ya kuona rasmi mitambo ikianza kazi ya kusawazisha eneo la ujenzi wa kituo hicho cha Afya ambapo serikali imeshatoa fedha 629,995,802/= kwa ajili ya ujenzi wake.

Rehema Emmanuel mkazi wa kata ya Vunta alisema kuwa, wamekuwa wakilazimika kutembea umbali mrefu kufuata huduma za Afya ambapo imekuwa changamoto kubwa kwao hasa wakinamama wajawazito.

“Hii ni neema kubwa sana kwetu hili ni jambo ambalo hatukuwai kuliwaza kutokea lakini leo ndoto yetu inatimia sijui tumlipe nini Rais Dkt. Samia na Mbunge wetu Anne Kilango kwa kazi hii kubwa ambayo wameifanya tunaamini Mwenyezi Mungu atawalipa kwa haya wanayotutendea” Alisema Rehema.

Naye Bruno Mzava mkazi wa kata ya Bwambo alisema kuwa, kujengwa kwa kituo hicho cha Afya kutasaidia kupunguza gharama za kufuata huduma za Afya ambapo apo awali walikuwa wakilazimika kutumia gharama kubwa kukodisha usafiri wa kuwafikisha wagonjwa katika kituo cha Afya cha Miamba.

Ikimbukwe kuwa, Mbunge wa Jimbo la Same mashariki, Anne Kilango Malecela alikuwa akililia ujenzi wa kituo hicho cha Afya kutokana na adha ambayo wananchi wake walikuwa wakikumbana nazo hali ilitopelekea Naibu Waziri Ofisi ya Rais na Serikali za mitaa (TAMISEMI) anayeshughulikia Afya, Dkt. Festo Dugange kufika katika kata hiyo mwaka juzi na kujionea jinsi wananchi wanapata adha na kudai Rais Dkt. Samia ameridhia ombi la kujenga kituo kipya cha Afya.

“Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan amesikia kilio chenu na kunituma kuja kujionea mwenyewe na ameniambia niwaambie kuwa ameridhia ombi lenu la kujengwa kwa kituo cha Afya na ameahidi kutoa fedha za ujenzi wa kituo hicho” Alisema Dkt. Dugange.


Related Posts