Taarifa zilizotolewa na Shirika la Habari la Uingereza (BBC) zinasema mwandishi wa mkongwe nchini ambaye aliwahi kuwa mtangazaji wa BBC, Ahmed Rajab amefariki dunia jana jioni huko London, Uingereza.
Ahmed pia aliwahi kuwa mwandishi wa habari wa Gazeti la Africa Event. Taarifa zaidi zinatarajiwa kutolewa baadaye na familia zikiwemo taratibu maziko.
Ahmed Rajab alijiunga na BBC mwazoni mwa miaka ya 1960. Baada ya kustaafu Ahmed Rajab alikuwa mmoja wa wachambuzi wa kutegemewa wa masuala ya kimataifa wa BBC.
Mara ya mwisho alifanya uchambuzi kuhusu mzozo wa Gaza Januari 30 mwaka huu.