Watekelezaji wa Mradi wa Tuinuke Pamoja, Mtandao wa Jinsia Tanzania (TGNP) na Aga Khan Foundation, wametoa mafunzo ya Uraghbishi kwa Waraghbishi kutoka ngazi ya jamii kutoka katika wilaya za Chemba, Kondoa TC, Kondoa DC, Mkoani Dodoma, Tanzania na maandalizi ya utekelezaji wa Uraghbishi katika ngazi ya jamii wenye lengo la kuimarisha uwezo na ujuzi wa Waraghbishi wa kutumia mbinu na nyenzo Shirikishi katika kuongoza na kuwezesha ujenzi wa tapo la Usawa wa Kijinsia na ukombozi wa Wanawake Kimapinduzi ngazi ya jamii yaliyoanza leo tarehe 04 hadi 07 Februari, 2025 Jijini Dar es salaam.
Akifungua mafunzo hayo Mkurugenzi wa Mtandao wa Jinsia Tanzania (TGNP) Lilian Liundi amesema lengo malengo ya mafunzo hayo ni kujenga uelewa wa dhana za jinsia na itikadi ya ukombozi wa wanawake kimapinduzi, Kukuza uelewa wa falsafa ya Uraghbishi kwa kutumia mbinu ya “U” tatu (Upimaji, Uchambuzi na Utekelezaji) kwa vitendo, Kuibua na kuchambua masuala ya kijinsia. wanawake-kwa kutumia mbinu na nyenzambalimbali za kiraghbishi, kuimarisha ujuzi wa uchambuzi na shirikishi (PAR) pamoja na utunzaji wa kumbukumbu na uwezo wa kuutumia katika utekelezaji ngazi ya jamii.
“Kwa mara ya kwanza na kipekee tumeona Mashirika makubwa katika ngazi ya kitaifa yamekuwa yakipokea ruzuku kutoka kwa wafadhili mara nyingi lakini kwa huu mradi ruzuku inakwenda mojakwamoja kwenye vikundi ili kurahisisha ile dhana ya kuwajengea uwezo” Alisema Liundi
Amesema mradi huu wa Tuinuke pamoja, unaofadhiliwa na Ubalozi wa Ireland nchini Tanzania, umelenga kuwawezesha wanawake wengi kwa sababu ndio wanaoathirika zaidi na masuala ya umaskini, ukatili wa kijinsia kwenye Nyanja ya uongozi inaonekana namba ni ndogo ya wanawake na hata kwenye kumiliki uchumi mwanamke bado kaachwa nyumba hivyo mradi huu utaweza kuwainua wanawake wengi ili waweze kufaidika na ndio maana wamepewa kiupaumbele kwenye huu mradi
Mkurugenzi Mtendaji wa Mtandao wa Jinsia Tanzania (TGNP) Lilian Liundi akifungua mafunzo ya Uraghbishi kwa Waraghbishi kutoka ngazi ya jimii katika wilaya za Chemba, Kondoa TC, Kondoa DC, Mkoani Dodoma yanayofanyika kwa siku nne katika ofisi za Mtandao wa Jinsia Tanzania (TGNP) zilizopo Mabibo jijini Dar es Salaam.
Meneja Mradi Tuinuke Pamoja Nestory Mhando akizungumza namna mradi utakavyofanya kazi katika wilaya za Chemba, Kondoa TC, Kondoa DC mkoani Dodoma wakati wa ufunguzi wa mafunzo ya Uraghbishi kwa Waraghbishi kutoka ngazi ya jimii yanayofanyika katika ofisi za Mtandao wa Jinsia Tanzania (TGNP) jijini Dar es Salaam.
Baadhi wa Waraghbishi na wafanyakazi wa Mtandao wa Jinsia Tanzania (TGNP) wakifuatilia hotuba ya Mkurugenzi Mtendaji wa Mtandao wa Jinsia Tanzania (TGNP) Lilian Liundi alipokuwa anafungua mafunzo ya siku nne ya Waraghbishi kutoka ngazi ya jimii katika wilaya za Mkoa wa Dodoma
Picha ya pamoja.