Donald Trump ni mfanyabiashara na mwanasiasa wa Chama cha Republican aliyechaguliwa kuwa Rais wa 47 wa Marekani akimshinda Kamala Harris wa Democrat. Trump aliapishwa kuingia Ikulu ya Washington DC, Januari 20, 2025. Lakini, tangu siku hiyo vuguvugu lake la mageuzi limetikisa mataifa mbalimbali dunia.
Trump alijizolea umaarufu uliompa ushindi kupitia kauli mbiu ya ‘Make America Great Again’ (Maga) akilenga kurejesha tena hadhi Marekani.
Kufuatia kauli mbiu hiyo, wapiga kura walitamani kufahamu mkakati wake wa kulifanya Taifa hilo kuwa taifa lenye nguvu zaidi duniani, kulimpa nafasi ya kuchaguliwa tena kwa kishindo.
Tofauti na uapisho wa marais wengine ambao hufanyika eneo la wazi Ikulu ya Washington DC, uapisho wa Trump ulifanyika ndani ya Jengo la Capitol-Rotunda na kuhudhuriwa na watu wachache wakiwemo marais wastaafu, mabilionea wa Marekani na wake zao.
Wananchi wengine walifuatilia uapisho huo kupitia mitandao ya kijamii na luninga. Trump aliapa akiwa ameshika Biblia iliyotumika kwenye uapisho wa Rais wa 16 wa taifa hilo, Abraham Lincoln mwaka 1861.
- Kuwafukuza wahamiaji Marekani
Saa chache baada ya kuapishwa, Rais Trump alianza kwa kusaini amri na sheria maarufu kama ‘Laken Riley Act’ inayoipatia mamlaka ikiwemo Idara ya Ulinzi wa Ndani (Homeland Security) kuanza kuwawinda na kuwarejesha makwao wahamiaji wasiyo na kibali cha kuishi nchini Marekani. Zaidi ya watu 1,445,549 wamefukuzwa.
- Jinsi mbili tu ndani ya Marekani
Achana na kuwafukuza wahamiaji, Trump alitangaza kuwa kuanzia Januari 20,2025, kutakuwa na jinsi mbili pekee nchini humo (mwanawake na mwanaume) huku akisitisha mafungu ya fedha zilizokuwa zikitumika kufadhili na kusaidia matibabu na ustawi wa watu waliobadili jinsi Marekani na duniani.
- Kusitisha ufadhili na misaada
Kilio kikubwa alichokileta hasa kwa mataifa machanga na masikini, ni uamuzi wa Trump kusitisha misaada na ufadhili akitangaza kufanyika kwa tathmini ya matumizi ya fedha za walipakodi wa Marekani.
Katika kutekeleza hilo, Trump alisitisha shughuli zote za Shirika la Marekani la Maendeleo ya Kimataifa (USAID), huku akiagiza tathmini ya uendeshaji wake na mifuko iliyoko chini yake ndani ya siku 90.
Pia, amesaini amri ya kuiondoa Marekani katika Baraza la Haki za Binadamu la Umoja wa Mataifa (UNHRC), Mpango wa Umoja wa Mataifa unaotoa Misaada kwa Wapalestina (UNRWA).
- Marekani yakiweka kando WHO
Ni uamuzi ulioishtua dunia baada ya Trump kutangaza kuliondoa taifa hilo katika Shirika la Afya Duniani. Marekani ndio mchangiaji mkubwa wa fedha za kuendesha WHO ikilinganishwa na mataifa mengine yenye idadi kubwa ya watu ikiwemo China. Tedros Adhanom Ghebreyesus, ambaye ni Mkurugenzi Mkuu wa WHO alisema uamuzi huo wa Trump utaathiri hali ya afya na ustawi wa watu duniani.
- Kuitwaa Guba ya Mexico, mfeleji wa Panama na Greenland
Turump ametangaza kuwa ataibadilisha rasmi jina la Guba ya Mexico kuwa Guba ya Marekani. Pia alitangaza mfereji wa Panama unaotumiwa na meli kufikisha mizigo katika taifa hilo kuwa makubaliano yalikuwa Marekani itaiachia Panama kuuendesha, lakini taifa hilo limebadili utaratibu na badala yake mfereji huo unaoendeshwa na China hivyo Marekani inauchukua tena.
Pia, ametangaza nia yake ya kubadili umiliki wa Visiwa vya Greenland vilivyoko chini ya usimamizi wa Denmark kuwa chini ya Marekani.
6. Vikwazo vya Mexico, Canada na China.
Katika kile alichodai ni kupambana na mataifa yanayopinga sera yake ya kuwaondoa wahamiaji, Trump alitangaza kuiwekea vikwazo Mexico, Canada na China. Vikwazo hivyo viliambatana na kuongezwa kwa Kodi ya Ongezeko la Thamani (VAT) ya asilimia 25 kwenye kila bidhaa inayoingia Marekani kutoka kwenye mataifa hayo.
Baada ya uamuzi huo, Rais wa Mexico, Claudia Sheinbaum na Waziri Mkuu wa Canada, Justin Trudeau walitangaza uamuzi wa kuiwekea vikwazo Marekani ikiwa ni kujibu mapigo. Mvutano huo ulimfanya Trump aibuke na kusitisha vikwazo alivyoweka kwenye bidhaa za mataifa hayo.
- Marekani kulichukua eneo la Gaza
Januari 4, 2025, Trump alitangaza mpango wa kuiwezesha Marekani kuchukua udhibiti wa eneo la Gaza na kuibadilisha kutoka magofu kuwa ‘Riviera’ yaani Pwani ya utalii ya Mashariki ya Kati.
Hata hivyo, mpango huo umepingwa vikali na mataifa ya kiarabu huku mwenyewe akisema mpango huo utatimia kwa kupeleka wanajeshi ikibidi huku akisisitiza kuondoka kwa Wapalestina wa Gaza na kwenye kutafuta hifadhi mataifa ya jirani.
Vipi unaoina wapi Marekani chini ya Donald Trump?