Makamu
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Philip Mpango na Mwenza
wake Mama Mbonimpaye Mpango wakitoa heshima za mwisho wakati wa kuaga mwili wa marehemu
Sekunda Massawe ambaye ni Mama mzazi wa Waziri wa Elimu Sayansi na Teknolojia
Mhe. Prof. Adolf Mkenda mara baada ya Ibada iliyofanyika katika Kanisa Katoliki
Parokia ya Mtakatifu Pius X – Tarakea mkoani Kilimanjaro. Tarehe 06 Februari
2025.
Makamu
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Philip Mpango akisaini
kitabu cha Maombolezo ya Msiba wa marehemu Sekunda Massawe ambaye ni Mama mzazi
wa Waziri wa Elimu Sayansi na Teknolojia Mhe. Prof. Adolf Mkenda alipowasili nyumbani
kwa familia hiyo Kijiji cha Nduweni Tarakea Wilayani Rombo Mkoani Kilimanjaro.
Tarehe 06 Februari 2025.
Makamu
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Philip Mpango akisaini
kitabu cha Maombolezo ya Msiba wa marehemu Sekunda Massawe ambaye ni Mama mzazi
wa Waziri wa Elimu Sayansi na Teknolojia Mhe. Prof. Adolf Mkenda alipowasili nyumbani
kwa familia hiyo Kijiji cha Nduweni Tarakea Wilayani Rombo Mkoani Kilimanjaro.
Tarehe 06 Februari 2025.
Makamu
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Philip Mpango akimfariji Waziri
wa Elimu Sayansi na Teknolojia Mhe. Prof. Adolf Mkenda kufuatia kifo cha Mama
yake marehemu Sekunda Massawe wakati alipowasili nyumbani kwa familia hiyo
Kijiji cha Nduweni Tarakea Wilayani Rombo Mkoani Kilimanjaro. Tarehe 06
Februari 2025.
Makamu
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Philip Mpango akitoa
salamu za rambirambi kwa waombolezaji mbalimbali mara baada ya Ibada ya kumuaga
marehemu Sekunda Massawe ambaye ni Mama mzazi wa Waziri wa Elimu Sayansi na
Teknolojia Mhe. Prof. Adolf Mkenda iliyofanyika katika Kanisa Katoliki Parokia
ya Mtakatifu Pius X – Tarakea mkoani Kilimanjaro. Tarehe 06 Februari 2025.
Makamu
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Philip Mpango na Mwenza
wake Mama Mbonimpaye Mpango leo tarehe 06 Februari 2025, wameungana na viongozi
na wananchi mbalimbali katika Ibada ya kumuaga marehemu Sekunda Massawe ambaye
ni Mama mzazi wa Waziri wa Elimu Sayansi na Teknolojia Mhe. Prof. Adolf Mkenda
iliyofanyika katika Kanisa Katoliki Parokia ya Mtakatifu Pius X – Tarakea
mkoani Kilimanjaro.
Akitoa
salamu za rambirambi kwa niaba ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe
Dkt. Samia Suluhu Hassan, Makamu wa Rais amesema Serikali,
inashukuru kwa maisha ya mama Sekunda ambaye alimzaa na kumlea Mhe. Prof. Adolf
Mkenda, Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia ambaye amekuwa Mtendaji na
Kiongozi mahiri katika utumishi wa umma, tangu alipokuwa anafundisha Chuo Kikuu
cha Dar es salaam na katika nafasi mbalimbali alizoshika Serikalini.
Amesema Taifa linaendelea
kufaidi matunda ya malezi bora na uchapakazi, ambayo mama Sekunda aliwapatia
watoto wake. Ametoa rai kwa wazazi na walezi kufanya kila jitihada kusomesha
watoto, kuwafundisha maadili mema, kushika dini yao kiadilifu, na kufanya kazi kwa
bidii kwa faida yao wenyewe, familia na Taifa kwa ujumla.
Makamu wa Rais amesema
kila mmoja anapaswa kujitahidi kuishi vema na binadamu wenzake na kufanya kazi
kwa bidii katika nafasi mbalimbali ili kutoa mchango mzuri kwa familia na
Taifa, na kuacha historia nzuri na mifano bora ya kuigwa na jamii. Ameongeza
kwamba ni muhimu kujiandaa kumrudia Muumba maana hakuna ajuaye siku wala saa.
Ibada ya kumuaga marehemu
Sekunda Massawe imeongozwa na Askofu wa Jimbo Katoliki Moshi Mhashamu Ludovick
Minde na kuhudhuriwa na viongozi mbalimbali wa Serikali wakiwemo Mawaziri,
Naibu Mawaziri, Makatibu Wakuu, Wakuu wa Mikoa, Wabunge, Viongozi wa Taasisi
mbalimbali, Viongozi wa Dini pamoja na
wananchi mbalimbali.