Taasisi zilizochini ya Wizara ya Ujenzi, Mawasiliano na Uchukuzi Unguja
na Pemba zajengewa uwezo juu ya Namna ya Utayarishaji wa Bajeti zenye
Vipaumbele vya Kijinsia katika Ukumbi wa ZMA Malindi.
Akifungua
Mafunzo hayo Afisa Mipango kutoka Wizara ya Ujenzi, Mawasiliano na
Uchukuzi kwa niaba ya Mkurugenzi Mipango, Sera na Utafiti wa Wizara hiyo
Zahra Nassor Said amesema lengo la kikao hicho ni kuwa andaa watendaji
wa Wizara hasa wanaotayarisha Bajeti za Mashirika na Taasisi zilizochini
ya Wizara ya Ujenzi katika Eneo la Utayarishaji Bora wa Bajeti, MTEF,
PBB pamoja na Bajeti yenye kuzingatia masuala ya Usawa wa Kijinsia ili
waweze kuendana na hali halisi ya Mipango mikuu ya Serikali.
Zahra
amewataka Watumishi hao kuwa Watulivu na Wasikivu kwani Bajeti yoyote
Itakayoandaliwa na Mashirika na Taasisi zilizo chini ya Wizara ya
Ujenzi, Mawasiliano na Uchukuzi kama hazikuzibgatia mahitaji
yaliyoainishwa na Wizara ya Fedha kupitia Tume ya Mipango na Kitengo cha
Bajeti cha Wizara ya Fedha na Mipango basi bajeti hiyo haitakuwa na
nafasi ya kupokelewa.
Akitoa Mada ya Namna Bajeti zitakazo
tayarishwa kuzingatia suala zima la Usawa wa Kijinsia. Afisa Bajeti
Kutoka Wizara ya Fedha na Mipango Mwanakhamis Mzee Hafidh amesema
kumekua na Utayarishaji wa Bajeti wa Kimazoea kwa muda mrefu
usiozingatia Kipaumbele cha masuala ya Usawa wa Kijinsia jambo
lililopelekea Kuachwa nyumba kwa jinsi moja dhidi ya nyengine. Jambo
hilo amesema Serikali imeliona na kwenye bajeti ya 2025/ 2026
watahakikisha linazingatiwa ili kujenga Jamii yenye Usawa wa kijinsia.
Ametolea
Mfano wa uwepo wa Idadi kubwa ya Wasarifu Majengo na Wakandarasi wa
kiume ukilinganisha na wa kike jambo linalopelekea kuachwa nyuma mno kwa
jinsia ya kike kwenye miradi mingi inayoendelea nchini.
Mwanakhamis
amewataka washiriki kuhakikisha wanatoa kipaombele kwa kila Kada
kujitokeza kwa masuala ya usawa wa kijinsia katika utayarishaji wa
bajeti zao.
Kwa Upande wake Fatma Mgeni Kombo Afisa Bajeti
kutoka Wizara ya Fedha na Mipango amezungumzia namna nzuri ya
Uandaajibwa MTEF na PBB kwa taasisi na kuzitaka zijielekeze kwenye
kuimarisha maeneo hayo kwa Taswira Njema ya Wizara ya Ujenzi,
Mawasiliano na Uchukuzi.
Mafunzo hayo ya siku Moja Yamefungwa
Rasmi na Afisa Mipango kutoka Wizara ya Ujenzi, Mawasiliano na Uchukuzi
kwa niaba ya Mkurugenzi, Sera, Mipango na Utafiti wa Wizara hiyo
Bi.Zahra Nassor Said na kuzishirikisha taasisi zote zilizo chini ya
Wizara ya Ujenzi,Mawasiliano na Uchukuzi Unguja na Pemba .