Ushindi wampa jeuri Minziro | Mwanaspoti

BAADA ya kuibuka na ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Dodoma Jiji ugenini, kocha mkuu wa Pamba, Fredy Felix ‘Minziro’ amesema ushindi na bonasi waliyoipata wachezaji ni chachu ya kuongeza ushindani kuelekea mchezo  dhidi ya Azam FC Jumapili.

Pamba Jiji baada ya kuibuka na ushindi dhidi ya Dodoma Jiji, Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, Said Mtanda amewakabidhi wachezaji Sh10 milioni kama motisha ya kuendeleza juhudi za kupambana kitu ambacho kimemuibua Minziro.

“Tuna mchezo mwingibne ugenini dhidi ya Azam FC naamini ushindi tulioupata na motisha iliyotolewa na Mkuu wa Mkoa itaongeza chachu ya ushindani kwa wachezaji. Hili linanipa imani kuwa tuitaingia kupambania pointi tatu tukiwa katika hali nzuri,” alisema na kuongeza:

“Tunaenda kukutana na timu bora na imara ambayo imekamilika kila idara hilo haliwezi kutupa shida kutokana na aina ya matokeo tuliyotoka kuyapata nina imani kubwa na wachezaji wangu wataingia kwenye mchezo huo wakiwa kwenye morali nzuri na watapambania vitu viwili tofauti.” Minziro alisema watakuwa na akili ya kupata matokeo mazuri kwa kukusanya pointi nyingine tatu ugenini ili kuendelea kupokea fedha kutoka kwa mkuu wa mkoa.

Related Posts