Dar es Salaam. Rais wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC), Felix Tshisekedi hajawasili kuhudhuria mkutano wa kujadili amani ya nchi hiyo badala yake atawakilishwa na Waziri Mkuu wake, Judith Suminwa.
Suminwa aliwasili Tanzania alfajiri ya leo Februari 8, 2025 kushiriki Mkutano wa Dharura wa Pamoja wa Wakuu wa Nchi na Serikali wa Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC) na Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC) utakaofanyika hapo baadaye.

Mkutano huo unafanyika huku vikundi vya waasi chini ya Alliance Fleuve Congo (AFC/M23) vikiwa vimekamata miji ya Goma, Kivu Kaskazini na Nyabibwe, Kivu Kusini vikielekea Bukavu.
Endelea kufuatilia Mwananchi.