Na Mwandishi Wetu
HALMASHAURI ya Wilaya ya Busokelo imefanikiwa kutoa mikopo ya asilimia 10 kama takwa la kisheria na maelekezo Rais Dk.Samia Suluhu Hassan kwa vikundi vya wanawake, vijana na watu wenye ulemavu.
Akizungumza kuhusu mikopo hiyo Mkurugenzi wa Halmashauri hiyo Dkt.Mwinyi Omary Mwinyi amesema jumla ya Sh.milioni 177 zimetolewa kwa vikundi hivyo Februari 6,2025 ikiwa ni awamu ya kwanza ya kutoa mikopo.
Aidha Dkt. Mwinyi ameeleza awamu ya pili imeanza kwa usaili wa vikundi mbalimbali kuanzia Februari 2 mpaka Februari 30 mwaka huu ambapo Sh.milioni 500 zinatarajiwa kutolewa kwa vikundi vitakavyopitishwa.