Wahitimu 25 Wakamilisha Mafunzo ya Kozi ya Uongozaji ndege Daraja la kwanza (Aerodrome Control Course)na Urubani wa Ndege Nyuki (Drone) katika Chuo cha CATC


Jumla ya washiriki 25 wamehitimu mafunzo maalumu ya anga katika Chuo cha Usafiri wa Anga Tanzania(CATC), hatua inayochangia kuimarisha sekta ya anga nchini Tanzania.

Washiriki 19 wamekamilisha Mafunzo ya Urubani wa wa Ndege Nyuki (Drone), huku wengine sita wakihitimu Mafunzo ya Uongozaji Ndege Daraja la kwanza (Aerodrome Control – ADC). Hafla ya kufunga mafunzo hayo iliongozwa na Mkuu wa Mafunzo wa CATC, Didacus Mweya, ambaye aliwapongeza wahitimu na kuwasihi waendeleze jina zuri la taasisi hiyo kwa weledi na uadilifu.

“Ninyi sasa ni mabalozi wa CATC. Tumieni ujuzi na maadili mliyojifunza hapa ili mchangie vyema katika sekta ya anga,” alisema Mweya.

Mafunzo ya Urubani wa ndege nyuki yanawapa washiriki ujuzi muhimu wa kuendesha na kusimamia ndege zisizo na ruban, sekta inayokua kwa kasi katika anga. Kwa upande mwingine, Mafunzo ya ADC yanawaandaa waongoza ndege kudhibiti miruko katika viwanja vya ndege kwa usalama na ufanisi.

CATC inaendelea kuwa kitovu cha mafunzo ya anga nchini Tanzania, ikitoa kozi zinazokidhi mahitaji ya sekta hiyo inayozidi kukua.

Related Posts