Chanzo msongo wa mawazo kuwa tatizo la familia nyingi

Katika familia kuna aina za misongo ya mawazo inayosababishwa na wanafamilia wenyewe na mingine inasababishwa na walio nje ya familia. Visababishi vyote hivi huwaathiri wanafamilia kwa namna moja au nyingine.

Visababishi vilivyo ndani ya familia hujulikana kama “family stressors”, wakati vile vinavyotoka nje ya familia huitwa “extra family stressors”. Matokeo ya visababishi hivi yaweza kuwa magonjwa mbalimbali kwa wanafamilia.

Ukosefu wa muda unaonekana kuwa tatizo kwa wanafamilia wengi, wengi huwahi sana kutoka nyumbani mapema asubuhi na kuchelewa sana kurudi, hakuna siku shughuli zimepungua au kwisha.

Hakuna aliyetayari kumpa mwingine muda wake, si mke wala si mume, kila mmoja yuko bize, kila mmoja anajitahidi kukamilisha vingi alivyonavyo katika muda kidogo alionao.

Hali hii imeondoa amani katika familia nyingi, nyingine hazikuweza kustahimili na kwa hiyo huvunjika.

Jinsi tunavyoweza kukabiliana na hili

Jaribu kuomba marafiki wa familia nyingine kuwasaidia katika yale wanayoweza kuwasaidia.

Kwa mfano, jirani au marafiki wanaweza kuwasaidia kufanya ununuzi, kuwachukua watoto kutoka shule, kwenye mazoezi ya mpira au kuwapeleka sehemu fulani.

Ikishindikana basi mnaweza kuajiri mtu ambaye ataweza kuwasaidia katika shughuli zile msizoweza kuzifanya na zisizo muhimu sana ninyi kuzifanya ili kuwaachia nafasi ya kufanya vile vilivyo muhimu.

Huyu anayeajiriwa anaweza kuwasaidia kufua, kuosha vyombo, kutunza bustani. Kipaumbele chako cha kwanza, uwe mke au mume ni lazima kiwe familia yako.

 Ili kuhakikisha una muda mzuri na familia yako, unaweza kupanga kupata likizo za mwezi au za mwisho wa wiki, likizo zitakazo kuweka mbali na marafiki, wafanyakazi wenzako, majukumu ya kazini, ili uweze kuweka macho, akili, na masikio yako kwa familia yako.

Wenzetu wa nchi za magharibi hupanga kwenda  likizo kwa kwenda katika uvuvi, uwindaji, au kucheza katika theluji. Najua mazingira yetu ni tofauti kidogo, lakini wenye mashamba au mifugo nje ya mji wanaweza kwenda huko.

 Likizo za mahotelini na katika makambi ambako watoto hupiga kambi na wazazi kushiriki michezo kama vile gofu siyo mwafaka sana kwa familia zinazotaka kuwa na muda mzuri kwa mambo muhimu.

Ndoa ni kazi ngumu, kutunza na kuendeleza uhusiano bora katika ndoa au katika familia ndiyo kazi yenyewe.

Utafiti uliofanywa na David Farell umeonyesha kuwa katika wanandoa waliofanikiwa katika uhusiano wao, wengi wamekuwa wakishiriki tabia tano kuu muhimu zifuatazo:

1-Ukweli na uhalisi kwa mwenza wako (mke/mume)

2-Heshima na utii kwa mwenza wako

3-Mwenza alihesabiwa kama rafiki mkubwa, sio tu kama mke au mume

4 -Utayari wa kusamehe na kusamehewa

5-Hamu ya kumfurahisha na kumsaidia mwenza.

 Ni matumaini yangu kuwa wote tunahitaji kutumia jitihada zetu ili tuyafanye haya katika familia zetu.

Visababishi vingi vilivyotajwa humu vinaweza kuboreshwa kwa kuboresha mawasiliano baina ya wanafamilia.

 Tenga na tafuta muda maalumu wa kuongea na kuwasiliana bayana na wanafamilia wote, siyo tu kuwa bize na kutumia muda wote kwa mambo yako mwenyewe, huu ni ubinafsi mkubwa.

 Jueni kutenganisha muda wa waajiri wenu na muda wa familia zenu. Nyumbani ni nyumbani, mahali kwa ajili ya familia ni nyumbani. Ofisini ni ofisini.

Familia nyingine zina siku maalumu katika wiki ambapo kila mmoja huelezea jinsi au pale alipoudhiwa na nini kifanyike.

Weka muda wa kujua nini wanawo wanafanya shuleni, nani anawasumbua na kuwaumiza (miili yao au hisia zao), kwa nini na wanafikiri nini.

Pata muda wa kupokea mawazo yao katika kuijenga familia yao, wewe siyo bosi wa familia, watoto nao wana nafasi tena bora zaidi, fahamu ni nani au nini kilicho ndani ya familia ambacho huwafurahisha, huwahuzunisha.

Baadhi ya vitu vinavyosababisha msongo wa mawazo katika familia

Mosi, kuzidiwa na majukumu na mmoja kutoyaelewa majukumu yake.

Pili, mgongano katika kuyatimiza majukumu ya kifamilia.

Tatu, upungufu katika kuyatekeleza majukumu ya kila mmoja.

Nne, ukosefu wa kupeana zawadi, vichochezi au vihamasishi pale mmoja anapofanya vema.

Saba, kutotoshelezwa kwenye tendo la ndoa.

Related Posts