Rais wa kwanza wa Namibia Sam Nujoma afariki – Global Publishers



Rais wa Namibia, Dkt. Nangolo Mbumba, ametangaza kwa huzuni makubwa kifo cha Rais wa kwanza wa Taifa letu, Dkt. Sam Nujoma, akiwa ameeleza kuwa chanzo kikuu cha kifo chake ni maradhi yaliyoendelea kumdhuru.

“Kwa mshtuko mkubwa, natangaza kifo cha Mwasisi na Rais wa kwanza wa Taifa letu, ambaye si tu alikuwa Baba wa Taifa bali pia nguzo ya ukombozi wa Namibia,” alisema Dkt. Mbumba katika taarifa aliyotoa.

Taarifa hiyo inaeleza kuwa Rais Nujoma alifariki asubuhi ya leo baada ya kuugua mara kwa mara.

“Ndugu zangu Wanamibia, pamoja na kaka na dada zetu kutoka bara la Afrika na ulimwengu wote, tunashuhudia kusimamishwa kwa safari ya taifa letu kutokana na upotevu wa Baba wa Taifa wetu,” aliongeza Dkt. Mbumba.











Related Posts